METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, October 20, 2016

WAFANYA BIASHARA ACHENI KUIPIGA CHENGA SERIKALI KWA KUKWEPA KULIPA KODI

Image result for wafanyabiashara
Na Woinde Shizza,ArushaWito umetolewa kwa jamii ili waweze kuwa na maisha bora wawe na shughuli za halali za kufanya zitakazo waingizia kipato,ili wasiwe tegemezi katika familia zao na jamii kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa na Jaggy Singh ambaye ni mkurugenzi mkuu wa ushirika wa Kimataifa wa wafanyabiashara Wakristo ( FGBMFI),ambapo amewataka watu kufanya shughuli zao katika misingi iliyo halali ,katika uadilifu na waepuke udanganyifu.

Singh amesisitiza kuwa lengo kuu la mkutano ni kuwaleta wafanyabiashara pamoja kubadilishana mawazo na changamoto wanazopitia,kuonyesha umuhimu wa kuishi maisha ya uhalisia na kufanya kazi kwa bidii zaidi,ambapo amewataka kuepuka udanganyifu wasiipige serikali chenga kwa kutokulipa kodi ,wafuate utaratibu na sheria za nchi.

Kwa upande wake raisi wa (FGBMFI) nchini Tanzania Injinia John Njau amesema ushirika huo wa wafanyabiashara wa Kimataifa hawajishughulishi na biashara peke yake bali wanahubiri Injili kamili kwa kutoa ushuhuda wa vitendo hata kama wafanyabiashara wengine hawaamini lakini wao wanatimiza wajibu.

Ameainisha kuwa nchini Tanzania kwa sasa wana matawi ya ushirika huo wa wafanyabiashara Wakristo yapatayo(7) ambayo ni kama ifuatavyo,

Mbeya,Mwaza,Shinyanga,Kilimanjaro,Arusha,Dar es-salaam,Manyara pamoja na Zanzibar ,na kwa upande wa Kimataifa kwa ujumla yapo 169,ambapo kila tawi linafanya kazi kutokana na taaluma walizo nazo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo John Majo ,ambaye pia ni mwenyekiti wa tawi la Arusha ,amesema kuwa ushirika huo wa wafanyabiashara wa Kikristo mtu yeyote anaruhusiwa kujiunga maadamu anajishughulisha ,awe ameajiriwa ,mfanyabiashara ,au mjasiriamali anaruhusiwa nia yao kuu ni kuwaleta pamoja ili wamjue Mungu zaidi pia

Aidha amewataka vijana wa kiume wasipende maisha ya urahisi bali wachape kazi kwa bidii,wajitume waache tabia mbaya ya kuwa tegemezi kwani wananguvu Mungu amewapa wazitumie ili kujiingizia kipato kwani itawajengea heshima katika jamii

“Unamkuta kijana yupo tu mtaani hataki kujishughulisha ukimtazama hana ulemavu wowote ,anapenda maisha ya kifahari na starehe lakini kazi hataki kufanya matokeo yake anajikuta amejiingiza kwenye mambo ya aibu na fedheha kubwa katika jamiii,inatuhuzunisha sana sisi kama wazazi badilikeni mjitume “alisisitiza John.

Katika Kongamano hilo la Kimataifa la kila mwaka wasemaji walikuwa sita ,ambao waliongozwa na rais wa( FGBMFI )kutoka nchini Nigeria Injinia ,Ifeanyi .H.Odedo ambaye anasimamia matawi madogomadogo 3500 nchini Nigeria
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com