Vyama
vinavyounda muungano unaotawala Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na vyama
vyengine vidogo vimekubaliana kuchelewesha uchaguzi wa mwezi ujao hadi
Aprili mwaka 2018 hatua itakayoyakasirisha makundi ya upinzani.
Kundi kuu
la upinzani nchini Congo halikuweza kupatikana mara moja kuzungumzia
uamuzi huo lakini tayari limeitisha mgomo wa taifa hapo Jumatano
kumshinikiza Rais Joseph Kabila kuachia madaraka mwishoni mwa muhula
wake hapo mwezi wa Disemba.
Kundi
hilo kuu la upinzani linaloongozwa la Etiene Tshisekedi limesusia
mazungumzo ya usluhishi wa kitaifa kwa hoja kwamba ni ni njama za Rais
Kabila kuendelea kun'gan'gania madaraka.
Mwezi
uliopita madazeni ya watu waliuwawa wakati wa maandamano ya siku mbili
mjini Kinshasa kupinga mipango ya kuchelewesha uchaguzi huo kwa kile
serikali inachosema matatizo ya kifedha na vifaa katika kuwaandikisha
mamilioni ya watu katika nchi kikubwa ya kimaskini.
Muda zaidi kwa dafatri la wapiga kura
Vyama
hivyo vimekubaliana hapo Jumamosi kutowa muda zaidi kwa daftari la
kuandikisha wapiga kura na kumuachia Kabila endelee kubakia madarakani
hadi uchaguzi huo uliocheleshwa utakapofanyika hayo ni kwa mujibu wa
chama kimoja kilichohudhuria mazungumzo hayo Union for Congolese Nation
(UNC).Wajumbe katika mazungumzo hayo yumkini wakaidhinisha uamuzi huo
hapo Jumatatu.
Rais wa
chama hicho cha UNC Vital Kamere anatarajiwa sana kuwa Waziri Mkuu kama
sehemu ya serikali ya mseto inayopendekezwa chini ya mazungumzo hayo.
Kabila
ambaye ameingia madarakani hapo mwaka 2001 kufuatia kuuwawa kwa baba
yake amesema ataheshimu katiba lakini hakufuta uwezekano wa kujaribu
kubadili sheria za nchi hiyo kumwezesha kuwania muhula mpya .
Hatari ya kukosa utulivu
Marais wa
nchi jirani za Rwanda na Jamhuri ya Congo walibadili katiba zao mwaka
jana ili kuwawezesha kuwania muhula wa tatu na wapinzani wa Kabila
wanasema wana hofu Kabila naye atafanya hivyo hivyo.
Mamia ya
watu pia wamekufa tokea mwaka jana katika nchi jirani ya Burundi baada
ya Rais Pierre Nkurunzinza kutaka kuwania muhula wa tatu madarakani na
kusinda katika uchaguzi ambao wapinzani wake wamesema ulikuwa kinyume na
katiba.
Mkuu wa
ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Congo ameonya wiki
iliopita kwamba mkwamo wa kisiasa unatowa tishio kubwa sana la kuifanya
nchi hiyo kukosa utulivu.
Mamilioni
ya watu wamekufa katika mizozo ya kanda kati ya mwaka 1996 na 2003 na
Congo katu haikuwahi na tajiriba ya kukabidhiana madaraka kwa amani. DW
0 comments:
Post a Comment