Na Dotto Mwaibale
WAMILIKI
wa magari wametakiwa kuchukua tahadhari ya kuzima na kufunga milango
magari yao pale wanaposimama kwa dharura kupata mahitaji mbalimbali ili
kuyanusuru kuibwa.
Mwito
huo umetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kamishna Msaidizi
wa Polisi (ACP), Suzan Kaganda wakati akizungumza na waandishi wa habari
Dar es Salaam kuhusu tukio la kuibwa kwa gari la Kapteni Innocent Dallu
maeneo ya Mbezi Juu huku akiwemo mtoto wake Lightness.
"Napenda
kutumia fursa hii kuwaomba wamiliki wa vyombo vya moto kuchukua
tahadhari ya kuzima magari yao na kufunga milango wanaposimama maeneo
yoyote kupata mahitaji yao kwani si rahisi kumbaini mhalifu kwani wapo
kila sehemu" alisema Kaganda.
Alisema
katika tukio la kuibwa kwa gari la kampteni Dallu alikuwa amesimama
maeneo ya Mbezi Juu bila ya kulizima akinunua mahitaji ambapo walitokea
vijana wakaondoka na gari hilo aina ya Toyota Harrier baada ya
kumtelemsha mmoja wa watoto aliyekuwemo ndani ya gari hilo aitwaye
Philip huku wakiondoka na mdogo wake Lightness.
Alisema
watuhumiwa hao walimtelekeza mtoto huyo maeneo ya Golden Bridge katika
baa moja na kisha kuondoka na gari hilo ambalo lilipatikana baada
kukamatwa na polisi Kiwangwa mkoani Pwani ambapo kijana mmoja Ezekiel
Daud anashikiliwa na polisi kwa mahojiano.
Alisema
ni vizuri wamiliki wa magari kuzingatia jambo hilo ili kuepusha matukio
kama hayo ambayo yanapoteza muda mwingi wa kuyatafuta kwani tukio kama
hilo lilitokea hivi karibuni maeneo ya Kinondoni ambapo wahalifu
waliweza kuiba gari aina ya Noah lililosimamishwa bila ya kuzimwa na
kuondoka nalo na alijapatikana mpaka leo hii.
0 comments:
Post a Comment