Naibu
Waziri, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia
Wambura (kushoto) akisalimiana na Afisa Mkuu wa Kampuni ya StarTimes Bw.
jana wakati alipokutana naye kwa ajili ya kujadiliana masuala
mbalimbali ya ushirikiano jana 10/10/2016 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura akiongea na wawekezaji wa Makampuni matatu kutoka China jana 10/10/2016 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya
Viongozi na watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
pamoja na wawekezaji wakifuatilia mazungumzo hayo jana 10/10/2016 Jijini
Dar es Salaam.
Naibu
Waziri, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia
Wambura (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wawekezaji
pamoja baadhi ya Viongozi na watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo jana 10/10/2016 Jijini Dar es Salaam.
Picha/Habari na Benedict Liwenga-WHUSM)
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura
amekutana na kufanya mazungumzo na wawekezaji wa makampuni matatu kutoka
China, lengo la ziara la wawekezaji
hao likiwa ni kufanya utafiti kujua ni namna gani Kampuni ya StarTimes
inapiga hatua katika kusaidia kukuza maendeleo katika sekta ya habari
Tanzania.
Katika
mazungumzo hayo yaliyofanyika jana Wizarani hapo, Mhe. Wambura amesema
kuwa Serikali iko mbioni kujenga Jengo Maalum kwa ajili ya shughuli za
Kiutamaduni (Cultural Complex) ambalo linatarajiwa kujengwa Bagamoyo na
ndani ya jengo hilo kutawekwa vitu mbalimbali vinavyohusu utamaduni wa
Tanzania.
Ameeleza
kuwa, Tanzania imekuwa ikishirikiana na China katika masuala mbalimbali
yakiwemo ya michezo, utamaduni na Sanaa ambapo baadhi wa wageni kutoka
China wamekuwa wakifika kutalii na kuwekeza,
lakini pia baadhi ya Watanzania nao wamekuwa wakipata fursa ya
kutembelea China kujionea maendeleo na kujifunza mambo mbalimbali.
“Tanzania
inapenda kushirikiana na China katika mambo mbalimbali kama vile
kutengeneza filamu, michezo na hata utamaduni, kwakweli ushirikiano huu
umekuwa wa manufaa kwetu sisi Watanzania kwani unapanua wigo wa kukuza
maendeleo”, alisema Mhe. Wambura.
Ameongeza
kuwa, Kampuni ya StarTimes ni moja kati ya Makampuni yaliyoisaidia
Tanzania kuhama toka Analojia kwenda Dijitali ambapo kampuni hiyo
iliweza kuwekeza nchini kwa kuleta ving’amuzi vyenye bei nafuu kiasi cha kumwezesha Mtanzania wa hali ya chini kumudu kununua na kuweza kupata habari kupitia runinga yake.
Aidha,
amewashauri wawekezaji hao kutengeneza makala mbalimbali zinazohusu
utamaduni wa Kitanzania kwa kushirikiana na Watanzania kwani inaweza
kuleta soko zuri ndani na nje ya nchi.
Kwa
upande wake Kiongozi wa msafara wa wawekezaji hao ambaye pia ni Afisa
Mkuu wa Kampuni ya Star Media (T) Ltd Bw. jana amesema kuwa, China
itaendeleza ushirikiano na Tanzania ambapo iko mbioni
kutoa nafasi kwa Watanzania kutoka Shirika la Utangazaji TBC na Wizara
kwenda kujifunza namna ya kutengeneza habari ikiwemo Makala na upigaji
picha ili taaluma hiyo ije kuwasadia wengine.
0 comments:
Post a Comment