Hatimaye
mbio za David Kafulila kupinga mahakamani matokeo ya uchaguzi wa ubunge
wa Kigoma Kusini ya Oktoba mwaka jana uliompa ushindi Husna Mwilima
(CCM) zimefika ukingongoni baada ya mahakama ya rufaa kutupilia mbali
maombi yake.
Jopo
la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa waliokaa mjini Tabora, jana
lilitoa maamuzi yake kuhusu rufaa ya Kafulila na kueleza kuwa
wameyatupilia mbali maombi hayo kwakuwa yamekosa nguvu yenye uhalali wa
Kisheria.
Aidha,
Mahakama hiyo ya Rufaa imemtaka Kafulila ambaye hakuhudhuria mahakamani
hapo, kulipa gharama zote za shauri hilo la madai namba 212 la mwaka
2016.
Akizungumza
baada ya maamuzi hayo ya Mahakama ya Rufaa, Mbunge wa Kigoma Kusini,
Mwilima alisema Kafulila alijua kuwa hakuwa na madai yoyote mahakamani
na kwamba alicholenga ni kumsumbua ili akose muda wa kuwatumikia
wananchi wake.
“Kafulila
alijua fika kuwa hakuna kesi ya yeye kukata rufaa. Lakini alikata rufaa
kunisumbua ili nikose muda wa kuwatumikia wananchi waliniingiza
bungeni,” alisema Mwilima.
Kafulila
alifungua shauri la madai namba 2 la mwaka 2015 katika Mahakama Kuu
Kanda ya Tabora, akipinga ushindi wa Mwilima. Katika shauri hilo,
Kafulila aliwalalamikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Msimamizi wa
uchaguzi na Husna Mwilima.
Mahakama
Kuu iliyatupilia mbali maombi ya Kafulila ya kutaka kutengua ubunge wa
Mwilima ndipo Mbunge huyo wa zamani wa Kigoma Kusini alipoamua kukata
rufaa katika Mahakama ya Rufaa ambayo ni Mahakama ya juu zaidi nchini.
Kesi
hiyo iliyovuta umakini wa wananchi wengi jimboni humo na huenda ndio
kesi ya uchaguzi iliyovuta watu wengi zaidi tangu kumalizika kwa
uchaguzi wa mwaka jana, imefikia ukingoni kwa kuhalalisha ubunge wa
Mwilima.
0 comments:
Post a Comment