Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha
ziara ya siku tatu nchini Zambia ambapo pamoja na mambo mengine alikuwa
ahudhurie sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya
Zambia Mhe.Edgar Chagwa Lungu ili aweze kushughulikia tatizo la tetemeko
la ardhi lililosababisha vifo vya watu 16 ,mamia wakiwa wamejeruhiwa na
nyumba kadhaa kubomolewa mkoani Kagera.
Kufuatia
kuahirisha ziara hiyo Mheshimiwa Rais Dkt.Magufuli amemtuma Makamu wa
Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kumuwakilisha katika sherehe hizo za
kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe.Edgar Chagwa
Lungu
Rais
Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu zinatarajiwa
kufanyika keshokutwa tarehe 13 Septemba, 2016 katika Jiji la Lusaka.
Jaffar Haniu
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi
Dar Es Salaam
11 Septemba, 2016
0 comments:
Post a Comment