Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mhe. Geprge simbachawene akisikiliza
maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF Bw. Sebera Fulgence
kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wanyakazi (WCF) alipotembelea banda la
Mfukohuo, pembezoni mwa mkutano mkuu wa mwaka wa ALAT mjini Musoma

MFUKO wa
Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), umetoa elimu kuhusu mambo
mbalimbali yanayohusu Mfuko kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu 32 na Tuzo za
viongozi wa SerikalI za Mitaa (Mayors Award), mjini Musoma mkoani Mara.
Mkutano
huo ulioanza Septemba 22 na kufunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene Septemba 23, 2016, unatarajiwa
kumalizika Septemba 24, 2016.
Akitoa
mada kwenye Mkutano huo juu ya shughuli na huduma zitolewazo na WCF,
Meneja Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Sebera Fulgence, (pichani juu),
alisema, Mfuko umeanza kutoa Fidia kwa Wafanyakazi tangu Julai mwaka
huu wa 2016 na kuwahimiza waajiri kupeleka michango yao kama ambavyo
Sheria iliyoanzisha Mfuko huo inavyoelekeza.
Wajumbe
wamepata uelewa na madhumuni ya uwepo wa Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi, majukumu yake, jinsi ya kuchangia na viwango vinavyotakiwa
kwa mwaka wa fedha 2015/2016 na 2016/2017.
Pamoja
na mambo mengine wamepata fursa ya kupata taarifa kwamba kupitia
Tangazo la Serikali Na 212A la tarehe 30 Juni 2016, Mfuko umeanza
kupokea madai na kulipa mafao kwa kuzingatia matakwa ya Sheria ya Fidia
kwa Wafanyakazi [Sura 263 marejeo yam waka 2015] ikisomwa pamoja na
Kanuni za Sheria ya Fidia kwa
Wafanyakazi za Mwaka 2016
Wafanyakazi za Mwaka 2016

Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Bw. Sebera juu ya kazi za Mfuko huo

Maafisa
wa WCF wakiwa kwenye banda la Mfuko huo pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa
mwaka wa ALAT. Kutoka kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo,
Sebera Fulgence, Athumani Khalfan na Zaria Mmanga, wakisubiwri kutoa
elimu kwa wajumbe kuhusukaziza Mfuko

Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Bw. Sebera juu ya kazi za Mfuko huo.
0 comments:
Post a Comment