METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, September 23, 2016

MASAUNI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA STENDI KUU UBUNGO NA KIBAHA, AGUNDUA MABASI MABOVU, AYAZUIA KUSAFIRI


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akishuhudia Dereva wa Basi la Tahmeed (kulia) akipimwa kilevi na Trafiki Nuru Mvungi kabla ya Basi lake kuruhusiwa na safari. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam pamoja na Kibaha mkoani Pwani jana. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mpa7
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari, Picha ya Ndege Kibaha, Pwani, mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kukagua mabasi mabovu na usalama wa abiria. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam pamoja na Kibaha mkoani Pwani jana. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, Bonaventura Mushongi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

mpa8
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akihoji usalama wa mtoto baada ya kugundua siti moja kukaa watoto wawili jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa abiria. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam. Na baadaye alielekea Stendi ya Kibaha kuendelea na ukaguzi huo wa mabasi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mpa9
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiwasalimia wananchi wa Picha ya Ndege, Kibaha mkoani Pwani mara baada ya kumaliza ukaguzi wa mabasi mabovu pamoja na madereva ambao hawana leseni. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam. Na baadaye alielekea Stendi ya Kibaha kuendelea na ukaguzi huo wa mabasi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mpa1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa tai) akielekea Stendi Kuu ya Mabasi ya mikoani Ubungo, jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza yenye lengo la kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria katika Stendi hiyo pamoja na Stendi ya Kibaha mkoani Pwani. Masauni alilizuia Basi la Shambarai lenye namba za usajili T419 BUF na Basi la Karachani (T253 CLZ) ambayo yalikuwa yanaenda Tanga kutokuendelea na safari zake kutokana na ubovu wa mabasi hayo ambayo yangeweza kuhatarisha maisha ya abiria. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mpa2
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwauliza abiria wa Basi la Harambee linalofanya safari zake Dar es Salaam kwenda Arusha, maswali mbalimbali kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo wakati wanaposafiri. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mpa3
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikagua mikanda katika Basi la Shambalai wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam jana. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mpa4
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akioneshwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga, tairi la Basi la Shambalai ambalo halina ubora kwa ajili ya kusafirisha abiria. Hata hivyo Masauni aliagiza basi hilo lizuiwe kufanya safari na pia kuchukuliwa hatua kali kwa Mmiliki wa basi hilo pamoja na Dereva. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mpa5
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa tai) akizungumza na madereva wa Basi ya mikoani pamoja na wa magari madogo ya mizigo yanayopaki Stendi Kuu Ubungo, jijini Dar es Salaam. Masauni aliwataka madereva hao kufuata sheria za usalama barabarani. Hata hivyo, madereva hao walilalamika kuwa hawana mikataba ya kazi zao. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi hiyo, jana. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com