Mkuu wa
mkoa wa Iringa Amina Masenza (kushoto) akimpongeza Salim Asas
(kulia) mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika miradi mikubwa
miwili iliyofadhili kampuni ya Asas ukiwemo mradi wa jengo la kituo
cha damu salama Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa na jengo la
watoto wanaozaliwa njiti yote yaliyofadhiliwa kwa zaidi ya Tsh milioni
400 na kampuni hiyo ya Asas ya mkoa wa Iringa(picha na
matukiodaimaBlog )
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akisaini kitabu cha wageni
Mkurugenzi wa kampuni ya Asas ya Iringa wa tatu kushoto akiwa katika Hafla hiyo
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa miradi hiyo
Mkuu wa
mkoa wa Iringa Amina Masenza ( wa tano kulia ) akiwa na mfadhiliwa
wa miradi ya jengo la kituo cha damu salama Hospitali ya Rufaa ya
mkoa wa Iringa Salim Asas kutoka kampuni ya Asas ya mkoa wa Iringa
(kulia kwake) pamoja na viongozi wengine walioshiriki Halfa ya uwekaji
wa mawe ya msingi katika mradi huo na jengo la watoto njiti yote
ikiwa na zaidi ya Tsh milioni 400 zilizotolewa na kampuni ya Asas wa nne kutoka kushoto ni mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akizindua majengo hayo kwa hotuba
Mkuu wa
mkoa wa Iringa Amina Masenza na mfadhili wa miradi ya jengo la Benki
ya damu na jengo la watoto njiti wakiweka jiwe la msingi leo
anayeshuhudia ni mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela
Mkuu wa mkoa wa Iringa akiwa ndani ya jengo la benki ya damu
Viongozi mbali mbali wakiwa na mkuu wa mkoa kukagua kituo hicho
Mkuu wa
mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa na mfadhiliwa wa miradi ya jengo
la kituo cha damu salama Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
Salim Asas wa nne kutoka kulia kutoka kampuni ya Asas ya mkoa wa
Iringa pamoja na viongozi wengine walioshiriki Halfa ya uwekaji wa
mawe ya msingi katika mradi huo na jengo la watoto njiti yote ikiwa
na zaidi ya Tsh milioni 400 zilizotolewa na kampuni ya Asas wa nne
kutoka kushoto ni mkuu wa wilaya ya Iringa Richard
Na MatukiodaimaBlog
SERIKALI
ya mkoa wa Iringa imepongeza msaada mkubwa uliotolewa na kampuni
ya Asas ya mkoa hapa wa ujenzi wa jengo la kituo cha damu salama
cha kisasa na ujenzi wa jengo la watoto wanaozaliwa njiti katika
Hospitali teule ya mkoa wa Iringa pamoja miradi itakayogharimu
zaidi ya Tsh milioni 400
Katika taarifa iliyosomwa na mganga mkuu wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa Dr Robert salim wakati
wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika miradi hiyo leo mbele
ya mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema kuwa
awali uongozi wa hospitali hiyo ulimwandikia barua
mfanyabiashara huyo ili kusaidia msaada wa kontena ambalo
lingetumika katika kituo cha benki ya damu salama ila mfanyabiashara
huyo alijitolea kujenga jengo hilo la kisasa na kuongeza msaada wa
jengo la watoto wanaozaliwa njiti .
“Kutokana na agizo la Serikali la kuanzisha Benki za damu salama katika Mikoa….. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na Mfadhili Salim F. Abri Mkurugenzi wa Kampuni ya ASAS ili ona
ni vyema kujenga jengo la Kituo Kidogo cha damu salama katika Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa ili kufikia azma hiyo. …Hospitali ilimuomba Mfadhili
huyo atoe msaada wa “Container” kwa ajili ya shughuli hiyo, lakini
Mfadhili kwa kuona umuhimu wa huduma ya damu salama katika Mkoa aliomba
apewe ramani ili ajenge kituo hicho badala ya
kutumia“Container”.”alisema
Dr
Salim alisema kuwa Hospitali hiyo kabla ya mfanyabiashara huyo
kujitolea ujenzi wa jengo hilo kituo cha kidogo cha damu salama
ulikuwa ukitegemea damu kutoka kituo cha kanda kilichopo mkoani
Mbeya ila sasa wataweza kukusanya damu kupitia kituo hicho.
Alisema
kuwa lengo la mradi huu ni Kuboresha upatikanaji wa huduma za damu
salama katika Mkoa wa Iringa kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya damu
salama katika Vituo vya kutolea huduma za afya na kupunguza vifo vya
Uzazi, Watoto wachanga, Watoto na Wahanga wa ajali za barabarani na kuwa
lengo la Mkoa kwa mwezi ni kukusanya chupa 784 na kwa mwaka ni chupa
9,413 (units).
Hata
hivyo alisema mahitaji ya damu kwa mwezi katika Mkoa ni chupa 700
(unit) na katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ni chupa 160-200 Units kwa
mwezi kuwa tangu kituo kianze kutumika mwezi Februari,2016 Mkoa
umekusanya chupa 2,065 (22%) hadi sasa.
“Tunakushukuru
mkuu wa mkoa kwa kukubali mwaliko wetu wa kuwa Mgeni Rasmi katika
hafla hii ya kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo
inayotekelezwa na Mfadhili wetu Salim F. Abri Mkurugenzi wa Kampuni ya
ASAS ya Iringa. Katika hafla hii fupi tutakuomba uweke jiwe la Msingi
katika Mradi wa jengo la Kituo Kidogo cha Damu Salama na Jengo la Wodi
ya Watoto wachanga vyote vikiwa ni hisani kutoka kwa mfadhili wetu
Salim F Abri “
Alisema kuwa ujenzi huo unafanywa namkandarasi
anayenga mradi huu ni Buyungu General Enterprise wa Iringa chini ya
usimamizi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambaye amechangia kuchora
ramani za jengo hili na kusimamia mradi mpaka ulipokamilika, mchango
wake kama angelipwa ni Tshs.13,939,200.00.
Na kuwa utekelezaji wa mradi
ulianza kutekelezwa mwezi Novemba, 2014 na umekamilika mwezi Agosti,
2015. Jengo limeanza kutumika mwezi Februari, 2016. Pamoja na kujenga
jengo hili Mfadhili pia ametoa msaada wa samani, mafriji makubwa 4 ya
kutunzia damu na Computer 1 wenye thamani ya Tshs.30,000,000.00.
Aidha,
Hospitali ya Vicenza ya Nchili Italia ilichangia Tshs. 800,000.00
kwaajili ya kusafisha eneo la ujenzi na Meneja wa Benki ya Damu Salama
ya Kanda Mbeya ametoa msaada wa Vitanda 2 vya kutolea damu, Mizani
(weighing scales) za kupimia uzito chupa za damu na Mzani 1 wa kupimia
watu wanaojitolea damu.
Alisema
Mpaka umekamilika mradi huu wa kituo cha damu salama umegharimu jumla
ya Tshs.154,880,000.00 bila samani na vifaa tiba kuwa faida kuwa ya
mradi huo uboresha utoaji wa huduma za damu salama kwa kuwa na eneo
kubwa la kufanyia kazi,Kupunguza malalamiko ya wananchi kwa kukosa damu
salama
Pia
Kuzuia maambukizi ya magonjwa ya VVU/UKIMWI, Hepatitis B na C na
Kaswende,Kupunguza vifo vya uzazi, watoto wachanga, watoto na wahanga wa
ajali vinavyotokana upungufu wa damu au kutokwa na damu
nyingi,Kupunguza gharama za kufuata damu salama umbali mrefu (Damu
salama Kanda Mbeya) na kuongeza kuwa Wanufaika zaidi ni Watoto, Watoto
wachanga, Mama wajawazito, Wahanga wa ajali za barabarani na jamii kwa
ujumla.
Dr
Salim alisema kupitia mradi huo wanategemea Kupunguza malalamiko ya
wananchi juu ya huduma isiyoridhisha ya damu salama katika Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa na Halmashauri na kukomesha tatizo la rushwa.
Kuhusu
mradi wa jengo la watoto wanaozaliwa njiti alisema kuwa Mpaka
utakapokamilika mradi huu unatarajiwa kugharimu jumla ya
Tshs.309,210,000.00 bila samani na vifaa tiba ambazo zote fedha za
mfadhili huyo kampuni ya Asas.
Akizungumzia
hatua ya familia yake kujitolea kujenga miradi hiyo mikubwa Asas
alisema ni kutokana na changamoto kubwa aliyoiona baada ya
kutembelea Hospitali hiyo na hata mmoja kati ya wanafamilia wake
kupoteza mtoto baada ya kuzaliwa njiti na kukosa chumba kwa ajili ya
kunusuru uhai wake.
Mkuu
wa mkoa wa Iringa Amina Masenza pamoja na kupongeza kampuni ya Asas
kwa kujitolea misaada hiyo bado aliomba wahisani wengine kuzidi
kujitolea kwa ajili ya maendeleo na kuwa kama mkoa unatambua mchango
mkubwa wa kimaendeleo unaofanywa na kampuni ya Asas pia mfanyabiashara
Rajan aliyepata kujitolea kujenga chumba cha kuhifadhia maiti
hospitalini hapo .
Awali
mkuu wa wilaya ya Iringa akimkaribisha mkuu wa mkoa kuweka mawe ya
msingi katika miradi hiyo alisema misaada anayoendelea kutoka Asas
si tu kwa CCM na serikali yake ila hata kwa vyama vya upinzani na
wakazi mbali mbali wa mji wa Iringa hivyo kutaka Halmashauri ya
Manispaa
0 comments:
Post a Comment