METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, September 18, 2016

DC NDEJEMBI AAMURU WENYEVITI WA MADALALI KUACHIWA HURU BAADA YA KUTIWA NGUVUNI WIKI ILIYOPITA

 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo



Na Mathias Canal, Dodoma

Madalali waliokuwa wanatoza Tozo kwa wakulima, kwenye geti la soko na kutoza tozo ya kila kila Tani ya mzigo iliyokuwa inaingia sokoni ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi alibaini kadhia hiyo ya ufisadi nyemelezi na kupiga marufuku biashara hiyo.

Katika tuhuma za ufisadi huo Mkuu huyo wa Wilaya aliagiza kusimamishwa Kazi na kukamatwa Wenyeviti wa madalali na na Kampuni ya Cargo Porters kwa mahojiano zaidi ili kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu fedha walizokuwa wakikusanya kuainisha matumizi yake.

Hata hivyo tangu Kutiwa nguvuni kwa viongozi hao kumekuwa na mahojiano kadha kutaka kujua namna bora ya ufanyaji biashara na namna watakavyoweza kufanya udalali bila kuathiri mapato ya soko hilo.

Tamko hilo la Mkuu wa Wilaya hiyo kutamka rasmi kuwafungulia kifungoni inajiri ikiwa ni zaidi ya Siku 10 sasa tangu viongozi hao walipo kamatwa kwa ajili ya mahojiano.

Pamoja na kuruhusu kuwa Huru kwa viongozi hao Dc Ndejembi amewataka kujisajili serikalini ili wawe na chama kinachotambulika kwa majina na vitambulisho vya Kazi ambavyo vitawapa fursa kuvivaa na kutambulika vyema wakati wote wanapokuwa kazini.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya ya Kongwa amewaruhusu kufanya Kazi yao ya udalali bure bila malipo hadi kufikia Mwezi wa kumi ambapo sasa watapaswa kulipa kodi kwa bodi ya Soko.
Madalali hao kwa sasa wamepigwa marufuku kutoza Tozo yoyote ndani ya soko hilo kama walivyokuwa wakifanya awali kwa kutoza getini, na kwa wakulima jambo ambalo lilikuwa kinyume na taratibu na sheria za ukusanyaji wa kodi.

Sambamba na hayo pia Dc Ndejembi amewataka madalali hao kuendelea kufanya Kazi kwa bidii ili kujipatia mapato na kuwasihi kuchangia madawati ili kunusuru wanafunzi ambao wanakaa chini katika Wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla.

Katika kuimarisha ufanisi wa Huduma bora za elimu madalali hao wameahidi mbele ya Mkuu huyo wa Wilaya kuwa hadi kufikia Mwishoni mwa mwezi Octoba watachangia Madawati 20 huku kampuni ya Cargo Porters yenyewe ikiahidi kutoa madawati 10.

Kupitia mchango huo wa madawati hayo Dc Ndejembi amewasihi wadau kuendelea kuchangia madawati ili kukamilisha kadhia ya madawati yaliyosalia kwa sasa kwani Wilaya hiyo ina upungufu wa madawati 500 mpaka hivi sasa.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com