Waandamanaji
wameingia barabarani nchini kote Ujerumani Jumamosi (17.09.2016)
kupinga mpango mkubwa sana wa kibiashara kati ya Ulaya na Marekani na
hiyo kuwa pigo jipya kwa mpango huo unnaopingwa.
Waandamanaji
wameingia barabarani nchini kote Ujerumani Jumamosi (17.09.2016)
kupinga mpango mkubwa sana wa kibiashara kati ya Ulaya na Marekani na
hiyo kuwa pigo jipya kwa mpango huo unnaopingwa.
Umma wa
watu umemiminika mjini Berlin halikadhalika Munich licha ya kunyesha kwa
mvua wakibeba mabango yenye kuwakilisha makundi kadhaa yanayopinga
utandawazi, mashirika yasio ya kiserikali,vyama vya kisiasa na vyama vya
wafanyakazi.
Roland
Suess kutoka kundi lenye kupinga utandawazi la Attac ameliambia shirika
la habari la AFP kwamba walikuwa wakitarajia watu 250,000 kujitokeza
katika miji mikubwa ya Ujerumani ambapo 80,000 wanatazamiwa kujitokeza
Berlin.Washiriki wamekuwa na mabango yenye kudai "demokrasia badala ya
TTIP" na "kugawana na sio kugawa".
Umoja wa
Ulaya na Marekani zilianza kujadili mpango huo wa Biashara na Uwekezaji
kati ya Ulaya na Marekani (TTIP) hapo mwaka 2013 kwa lengo la kuanzisha
soko huru kubwa kabisa la biashara duniani lenye walaji milioni 850.Duru
mpya mazungumzo inatarajiwa kuanza mwezi wa Oktoba na Rais Barack Obama
wa Marekani anataka makubaliano yafikiwe kabla ya kuondoka madarakani
hapo mwezi wa Januari.
Mkataba
mwengine mdogo kama huo kati ya Ulaya na Canada ujulikanao kwa jina la
CETA pia unaendelea kushughulikiwa na unatarajiwa kutiwa saini hapo
mwezi wa Oktoba.Wafanyabiashara wenye kusafirisha nje bidhaa zao
wanauunga mkono mkataba huo kwa kuwa umeahidi ushuru mdogo ,kupunguza
urasimu na kutanuwa wigo wa walaji kwa bidhaa zao.
Upinzani Ulaya
Lakini
wajumbe katika mazungumzo hayo wamekabiliwa na upinzani Ulaya ambapo
walaji wamekuwa wakihofu kwamba kutaathiri soko la ajira la nchi
wanachama 28 wa umoja huo na viwango vya mazingira jambo litakalopelekea
upunguzaji wa gharama ambao nao utasababisha kupotezwa kwa ajira.
Suala
jengine tata ni mpango wa kuanzisha mahakama maalum kusikiliza kesi
zinazowasilishwa na kampuni dhidi ya hatua za serikali kukiuka masuala
ya miundo jambo ambalo wanaoupinga mkataba huo wanasema inawapa
makampuni kura ya turufu dhidi ya sera za serikali Jennifer
Morgan mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Greenpeace amesema
"CETA na TTIP inatishia ulinzi wa mazingira na walaji kwa mamilioni ya
watu barani Ulaya na Amerika Kaskazini."
Sio wananchi tu wanatofautiana
Sio tu
watu wa Ulaya waliogawika kuhusu makubaliano hayo yanayopendekezwa hata
serikali nazo zinatafautiana.Serikali ya Ufaransa imeweka upinzani mkali
ambapo Waziri Mkuu Manuel Walls akidai kukomeshwa kwa mazungumzo hayo
wakati kiongozi wa taifa lenye nguvu kubwa za kiuchumi barani Ulaya
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ameelezea kuunga mkono makubaliano
hayo.
Katika
mahojiano ya hivi karibuni Merkel ametaja suala la kiwango kikubwa cha
ukosefu wa ajira katika nchi kadhaa za Umoja wa Ulaya ambapo amesema :
"tunapaswa kufanya kila tunachoweza kuzalisha ajira ......makubaliano ya
biashara huru ni sehemu ya jambo hilo."
Lakini
hata ndani ya serikali ya mseto kuna upinzani kwa makubaliano hayo
yanayopendekezwa ambapo Naibu Kansela wa chama cha SPD mwezi uliopita
ametangaza mazungumzo hayo ya TTIP " ni kama vile yameshindwa."Sigmar
Gabriel ambaye ni waziri wa uchumi pia amesisitiza kwamba watu wa Ulaya
lazima wasikubali kuridhia madai ya Wamarekani.
Kwa
mujibu wa uchunguzi wa maoni wa hivi karibuni wa taasisi ya Ipsos
asilimia 28 ya wale walioulizwa wana mashaka iwapo biashara huru inaweza
kuwa na manufaa.Zaidi ya nusu yaani aslimia 52 wanasema itasababisha
viwango dhaifu na kuongeza bidhaa zizizokuwa na ubora.
DW
0 comments:
Post a Comment