Dawa ya jino bila kung’oa
Maumivu ya jino ni moja ya maumivu mabaya sana kuyapata, maumivu mengine
mabaya zaidi ni maumivu ya sikio. Jino linaweza kupatwa na maumivu
ambayo yanaweza kupelekea jino kutoboka na hata kuong’olewa kabisa. Dawa
zifuatazo zinaweza kutuliza maumivu ya jino na hata kuliziba kabisa
iwapo tayari limeanza kutoboka.1. Asali yenye mdalasini
Chukua asali vijiko vidogo vitatu na uchanganye na mdalasini ya Unga
kijiko kikubwa kimoja. Pakaa mchanganyiko huu kidogo kidogo juu ya jino
linalouma kutwa mara 3
2. Aloe vera (mshubiri)
Pata aloe vera fresh na uchane kupata maji maji yake (utomvu) na unyunyize juu ya hilo jino linalouma kidogo kidogo kutwa mara 2
3. Mafuta ya nazi na karafuu
Chukua karafuu 3 zitwangwe kwenye kinu, changanya na mafuta ya asili ya
nazi kijiko kidogo kimoja uliyotengeneza mwenyewe nyumbani. Pasha
kwenye moto kama dakika tatu, ipua na usubiri mchanganyiko wako upoe.
Paka mchanganyiko huu juu ya jino linalouma na uache kwa dakika 7 kisha
jisukutue kinywa na maji.
Thursday, September 29, 2016
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Na. Antonia Mbwambo, Arusha. Watumishi wa Umma nchini wamehakikishiwa kuboreshewa mazingira ya kazi kadri uchumi utakavyoruhusu ili kuleta ...
-
Mmoja wa Viongozi wa kikundi cha Hamasa cha Timu ya Tanzania Prison Stephen Rheda (aliyesimama) akitoa nasaha za mwisho kwa washabiki wenzie...
-
Nimebahatika kupata fursa kadhaa kukaa na kuzungumza na Mheshimiwa Rais Mstaafu Hayati Benjamin William Mkapa enzi za uhai wake....
-
Na Debora Charles (Mtakwimu) Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini na kuchapisha na kusamba...
-
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, David Cleopa Msuya, wakati alipomtembelea nyumbani kwake Upanga, jijini Da...
Powered by Blogger.

0 comments:
Post a Comment