Katibu
Mkuu Wizara ya Maji, Inj. Mbogo Futakamba na Mtendaji Mkuu wa Tanzania
Water Partnership, Dkt. Victor Kongo wakibadilishana Hati za Makubaliano
ya Utunzaji na Usimamizi wa Rasilimali za Maji nchini mara baada ya
kutia saini.
Wajumbe
walioshiriki katika kikao cha kutia saini Hati ya Makubaliano ya
Utunzaji na Usimamizi wa Rasilimali za Maji nchini kati ya Wizara ya
Maji na Umwagiliaji na Tanzania Water Partnership.
Meneja
Mipango, Andrew Takawira (kushoto) na Afisa Mipango, Michael Raamano
kutoka Taasisi ya Global Water Partnership ya Afrika ya Kusini walikuwa
ni miongoni mwa wajumbe wa kikao hicho.
Mtendaji
Mkuu wa Tanzania Water Partnership, Dkt. Victor Kongo akizungumza,
kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji, Hamza Sadiki na Katibu Mkuu
Wizara ya Maji, Inj. Mbogo Futakamba.
Katibu
Mkuu Wizara ya Maji, Inj. Mbogo Futakamba akiwa pamoja na Wakurugenzi wa
Wizara ya Maji na Umwagiliaji, wajumbe wa Global Water Partnership na
Tanzania Water Partnership mara baada ya kikao cha kusaini Hati za
Makubaliano ya Utunzaji na Usimamizi wa Rasilimali za Maji nchini.
Wizara ya
Maji na Umwagiliaji leo imesaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano
kati yake na Shirika lisilo la Serikali, Tanzania Water Partnership
(TWP) kwa ajili ya utekelezaji wa Utunzaji na Usimamizi wa Rasilimali za
Maji nchini.
Makubaliano
hayo yalisainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Mbogo Futakamba
na Mtendaji Mkuu wa Tanzania Water Partnership, Dkt. Victor Kongo na
kuhudhuriwa na wataalamu kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na wajumbe
kutoka Tanzania Water Partnership.
0 comments:
Post a Comment