METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, August 29, 2016

Rousseff apigani kurudi madarakani nchini Brazili

Dilma
Dilma Rousseff rais aliyesimamishwa nchini Brazil

Rais wa Brazil ambae amesimamishwa, Dilma Rousseff, amewaambia maseneta kuwa yeye ni mhanga wa njama za kisiasa, zilizopangwa na wale ambao aliwashinda katika uchaguzi mkuu miaka miwili iliyopita.

Amesema faida za kijamii za muongo mmoja uliopita zilikuwa hatarini.

Rousseff anachunguzwa na ma seneta katika hatua za mwisho za mashtaka yanayomkabili huko Brasilia.

Anatuhumia kwa kuipindisha bajeti ya nchi kuelekea uchaguzi mkuu.

Kumekuwa na maandamano yanayomuunga mkono Rousseff katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Katika mji wa Sao Paulo, polisi wametumia gesi ya machozi kuwatawanya waandamaji.apo rubo tatu ya maseneta watapiga kura dhidi yake mwishoni mwa juma, basi Rousseff ataondoka madarakani moja kwa moja.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com