METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, August 14, 2016

MUSSA HASSAN MGOSI ASTAAFU SOKA


 Mshambuliaji mwenye mashuti makali wa timu ya soka ya Simba ya Dar es Salaam, Mussa Hassan Mgosi, akiwa amembeba mtoto wake, mara baada ya kucheza dakika tatu, za kuaga kucheza soka kwenye pambano la soka la kirafiki baina ya timu yake na URA ya Uganda kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, Agosti 14, 2016. Mgosi baada ya kuchezea Simba kwa misimu 10 amestaafu soka na sasa atakua meneja wa timu hiyo. Miongoni mwa watu waliohudhuria sherehe hiyo ya kustaafu kwake, ni pamoja na Familia yake, mkewe Jasmin na watoto wake watatu. Katika pambano hilo la kirafiki baina ya Simba na URA, matokeo yamekuwa sare ya kufungana magoli  1-1. (PICHA NA K-VIS B;LOG/KHALFAN SAID)
gosi
 Mgosi akikokota mpira mbele ya mchezaji wa URL kwenye pambano la soka la kirafiki kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, Agosti 14, 2016

 Familia ya Mgosi ikiongozwa na mkewe Jasmina, (katikati) na watoto wake, Amina (kushoto) na Hassan wakipiga makofi baada ya Mgosi kustaafu soka kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam

 Mchezaji wa Kimataifa wa Simba, Laudit Mavugo, akiipasua ngome ya URL

 Ibrahim Ajib, akikokota mpira

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com