Mama Sara
Mmbaga (pichani) anatafutwa na Mtoto wake kipenzi kwani amepotea tangu
mwaka jana Oktoba 26, 2015 huku juhudi kubwa ya kumtafuta inayofanywa na
Binti yake Sarafina aliyepo nchini Marekani, ndugu na jamaa zikiwa bado
hazijafanikiwa.
Mara ya
mwisho Mama Sara Mmbaga alionekana maeneo ya Mbezi Makonde, Mtaa wa
Bunge Road, Jijini Dar e Salaam akiwa ameongozana na Mwanaume
ajulikanaye kwa jina la Gamaeli Mwasumbi maarufu kwa jina la “Gama”
mwenyeji wa Mbezi Beach.
Tangu
siku hiyo ya Jumapili tarehe 26 Oktoba, 2015 alitoweka kusikojulikana
huku vitu vyake vilivyokuwepo kwenye nyumba yake aliyokuwa anaishi
vikiwa vimeondolewa.
Aidha,
Juhudi mbalimbali za kumtafuta mama Sara Mmbaga zimefanyika bila
mafanikio tangu alipopotea ambapo taarifa ya kupotea kwake ziliripotiwa
katika Kituo cha Polisi Kawe pamoja na vituo mbalimbali vya Habari hapa
nchini.
Tunaomba watu, mtu yeyote atayeweza kumuona basi anaweza kutoa taarifa kituo cha Polisi kilichokaribu naye.
Tunajua
ni jinsi gani maumivu anayoyapata Mtoto wake kipenzi wa pekee Sarafina
lakini tunamuombea kwa Mungu amlinde huko aliko na Malaika wake
wamrudishe Mama Sara akiwa salama salimin kwenye himaya yake.
0 comments:
Post a Comment