MKUU
wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela (pichani) amesema amekwisha zungumza na
makundi mbali mbali ya vijana katika wilaya ya Iringa na kukubaliana
kutoshirikia maandamano ya umoja wa kupinga udikteta Tanzania
(UKUTA) japo anayehitaji kuandamana ruksa ila aandamane ndani ya
nyumba yake kuzunguka kitanda na sio kutoka mitaani.
Akizungumza
na vijana katika ukumbi wa Highlands mjini hapa wakati wa uzinduzi wa
Filam ya Figisu ya Ndoa ,mkuu huyo alisema kuwa vijana
wanapaswa kufanya kazi za kuwapatia kipato na sio kutumikishwa
kufanya maandamano hayo ambayo kwao hayana faida yeyote .
"Tumejipanga
kuwashughulikia wote watakakaidi agizo la serikali kuhusu
maandamano ya UKUTA ......kama mtu yeyote ana hamu ya kufanya
maandamano afanye ndani ya nyumba yake kuzunguka kitanda chake na
sio nje mara baada ya kumaliza kufanya maandamano ndani kwake
anapotoka nje ni kwa ajili ya kwenda kufanya kazi itakayomuigizia
kipato na sio kwenda vijiweni ama kwenye maandamano ya UKUTA ole
wake mtu akutwe akiandamana ama kupanga kuandamana "alisisitiza
Kasesela
Kuwa
serikali iliyopo madarakani ni serikali yenye uchungu na maisha ya
watanzania na kuwa moja katika ya mikakati yake ni kuona kila
mtanzania anakuwa na maisha bora na hakuna njia ya mkato ya
kuyafikia maisha bora zaidi ya kufanya kazi na sio kutumika kufanya
maandamano ya kuvutana na serikali .
Mkuu
huyo wa wilaya alisema amekwisha pata taarifa za mmoja kati ya
viongozi wa Chadema ambaye ameendelea kuhamasisha vijana kufanya
maandamano kwenye maeneo mbali mbali ya wilaya hiyo na kuwa mipango
yote tayari ameipata hatua mbali mbali kuchukua hatua dhidi ya
kiongozi huyo zinafanyika japo alisema mpango wao huo katika wilaya
ya Iringa hautafanikiwa .
"
Wakati serikali imezuia mtu ama chama chochote cha siasa
kufanya mikusanyiko siku ya Septemba mosi mwaka huu yupo mmoja kati
ya viongozi wa Chadema ambaye anaendelea kusambaza ujumbe kwa ajili
ya kuandaa maandamano ya UKUTA .....nasema hakuna aliyejuu ya
sheria tutashughulika na uvunjaji huu wa sheria unaofanywa na
kiongozi huyo"
Aidha
aliwataka vijana kutokubali kuingizwa katika matatizo na kiongozi
mmoja mwenye lengo baya dhidi yao na badala yake kupuuza wito
wake na kuendelea na shughuli zao za kila siku .
Kasesela
alisema amepata kufanya vikao na makundi mbali mbali kwa
kuwashirikisha baadhi ya madiwani wa kata mbali mbali wakiwemo wa
Chadema na wameapa kutoshiriki maandamano hayo .
0 comments:
Post a Comment