METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, August 4, 2016

Kundi la Boko Haram lagawanyika

Abubakar Shekau
Abubakar Shekau
Kiongozi anayepigwa vita wa kundi la Boko Haram amesema kuwa bado ndiye anayeliongoza kundi hilo licha ya taarifa ya kundi la Islamic State kwamba ameng'olewa mamlakani.

Abubakar Shekau alipuuzilia mbali uamuzi wa IS kwamba Abu Musab al-Barnawi ndiye kiongozi mpya wa kundi hilo.

Shekau amemshtumu al_Barnawi kwa kujaribu kufanya mapinduzi dhidi yake.

Kundi la Boko Haram linapigania kuipindua serikali ya Nigeria ili kutangaza serikali ya Kiislamu katika eneo la kaskazini mwa taifa hilo.

Katika kipindi cha miezi 18 iliopita,kundi hilo limepoteza eneo kubwa lililokuwa likidhibiti baada ya kukabiliwa vilivyo na jeshi la Nigeria na majirani zake.BBC
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com