METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, August 16, 2016

Balozi wa Israel Atembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete

JANA1
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi (kulia) akimkaribisha Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan wakati alipotembelea taasisi hiyo jana.
JANA2
Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan akisikiliza ripoti ya shughuli za kitibabu zinazotolewa na taasisi hiyo kutoka kwa Profesa Mohamed Janabi.
JANA3
Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi (kulia) wakiingia katika chumba cha upasuaji jana katika taasisi hiyo.
JANA4
Kaimu Mkurugenzi Huduma za Upasuaji JKCI, Dk Bashir Nyangasa akifafanua jambo kwa balozi huyo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.

JANA5
Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan akizungumza na madatari, wauguzi na wataalamu wengine wa taasisi hiyo jana.
JANA6
Madaktari, wauguzi na wataalamu wengine wakimsikiliza Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan jana kwenye taasisi hiyo.
JANA7
Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan (kulia) akisaini kitabu cha wageni kabla ya kupata taarifa fupi ya taasisi hiyo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi.
JANA8
Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan akizungumza na madatari, wauguzi na wataalamu wengine wa taasisi hiyo jana.
JANA9
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akizungumza kwenye mkutano huo jana.
JANA10
Dk Peter Kisenge akimkabidhi zawadi balozi huyo jana.
JANA11
Wafanyakazi wa taasisi hiyo wakiwa katika picha pamoja jana.

Na John Stephen

Dar es Salaam, Tanzania. Balozi wa Israel nchini Kenya, Yahel Vilan jana ameitembela Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na kuahidi kutoa mafunzo kwa wataalamu wa taasisi hiyo.

Balozi huyo ametembelea chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu na vyumba vya upasuaji pamoja na kuwaona wagonjwa wodini.

“Nimefurahishwa kusikia kuna madaktari ambao wamesoma Israel na ninapenda kuwaahidi kuwa Serikali yangu itaendelea kuisaidia tasisi hii, lakini sitatoa hela,” amesema jana.

Pia amesema kuwa anafarijika kuona shughuli za kitabibu zinazofanywa na taasisi hiyo kwa kuwa amekuwa akitaka kwenda kuitembelea lakini hakuwahi kupata nafasi hivyo amefurahi kupata fursa  hiyo.

Wakati huo huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Profesa Mohamed Janabi amesema wanakabiliwa na upungufu wa wataalamu sawa na asilimia 50.

“Tunahitaji wataalamu 278, sasa tuna wataalamu 147 kwa mfano tuna wauguzi 96, mahitaji halisi ni wauguzi 150,” amesema Profesa Janabi.

Katika hatua nyingine, Profesa Janabi amesema hospitali hiyo tayari imewafanyia upasuaji zaidi ya watoto 600 kuanzia mwaka jana hadi sasa.

Profesa Janabi amesema taasisi hiyo imewekeza zaidi katika kununua vifaa tiba vya kisasa na kuwawezesha madaktari na wauguzi kupata mafunzo kutoka nje ya nchi ikiwamo Israel.

 Amesema kuwa mpango huo umesaidia wagonjwa wengi kufanyiwa upasuaji  ambao umekuwa ukifanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90.

Baadhi ya wageni waliowahi kutembelea taasisi hiyo ni mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania, mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria na mchezaji wa kimataifa,  Nwankwo Kanu na madaktari kutoka  nchi mbalimbali ambao wamekuwa wakishiriki katika upasuaji.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com