Tottenham walifanikiwa kupata ushindi dhidi ya Swansea 2-1 na kusalia katika nafasi ya pili wakiwa na alama 54 tatu zaidi ya The Gunners.
”Kwa hakika hatuwezi kujihurumia eti kwa sababu tuliambulia kichapo Old Trafford ,lazima tujifurukute na kuthibitishia wapinzani wetu kuwa tupo kwenye kinyang’anyiro cha kombe la ligi msimu huu.” alisema Wenger.
Arsenal wanaialika Swansea ambayo ipo nafasi ya 16 katika jedwali la ligi ya premia ya Uingereza uwanjani Emirate.
Huku zikiwa zimesalia mechi 9 pekee msimu huu ukamilike kila mechi na alama inaumuhimu mkubwa katika vilabu husika.
Wenger alisema ” Kimsingi kichapo hicho kina maana zaidi ya moja kwetu,,,matokeo kamili yatabainika mwisho wa msimu.
Wenger hata hivyo alikataa katakata kukubali kuwa walishindwa na kikosi cha chipukizi cha United.
”tangu lini De Gea amekuwa mchezaji chipukizi, hawa wachezaji waliigharimu United mamilioni ya pauni, Watizame Memphis Depay, Morgan Schneiderlin na Juan Mata hicho ni kikosi dhabiti.”alinuna Wenger
Jiunge na Bongo5.com sasa Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!
0 comments:
Post a Comment