ri Nape kunogesha Tamasha la Pasaka
WAZIRI
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, anatarajia kuwa
mgeni rasmi kwenye Tamasha la Pasaka litakalofanyika jijini Mwanza Machi
27.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo,
Alex Msama, kamati yake inaendelea na maandalizi ya kuelekea tamasha
hilo ambalo litashirikisha waimbaji mbalimbali hapa nchini.
“Maandalizi kuelekea Tamasha la Pasaka yanaendelea vema, hivyo wakazi
wa mikoa ya Kanda ya Ziwa wajiandae kupokea ujumbe wa neno la Mungu
kupitia viongozi wa dini na waimbaji wa muziki wa Injili,” alisema
Msama.
Msama alisema baadhi ya waimbaji wamethibitisha kushiriki tamasha
hilo ambao ni pamoja na Rose Muhando, Bonny Mwaitege, Upendo Nkone,
Jesca BM Honore, Christopher Mwahangila, Joshua Mlelwa, Sifael Mwabuka,
Jenipher Mgendi, Kwaya ya AIC Makongoro na Kwaya ya Wakorintho Wapili.
0 comments:
Post a Comment