Clinton ameshinda majimbo matano
Mgombea
wa Democratic Hillary Clinton na mgombea wa Republican Donald Trump
wamechukua uongozi wa mapema katika mchujo wa kuteua wagombea urais
Marekani katika vyama vyao.
Wagombea wote wawili wameshinda majimbo ya Alabama, Georgia, Tennessee na Virginia.
Bw Trump hata hivyo ameshindwa na Seneta Ted Cruz majimbo ya Texas na Oklahoma.
Mgombea wa Democratic Bernie Sanders naye ameshinda kwake nyumbani katika jimbo la Vermont na pia katika jimbo la Oklahoma.
Donald Trump anaongoza chama cha Republican
Mchujo wa
Jumanne Kuu hushuhudia majimbo 11 yakifanya mchujo kwa pamoja huku
maandalizi ya uchaguzi mkuu tarehe 8 Novemba yakiendelea kushika kasi.
MOJA KWA MOJA: Mchujo wa Jumanne Kuu Marekani
Bi
Hillary Clinton, aliyekuwa wakati mmoja waziri wa mashauri ya kigeni wa
Marekani, pamoja na mfanyabiashara tajiri kutoka New York Donald Trump
walipigiwa upatu kushinda majimbo mengi Jumanne Kuu.
Bi Clinton pia ameshinda Arkansas na Texas, naye Bw Trump akashinda Massachusetts.
Utafiti
wa maoni ya paada ya kura unaonyesha Trump na gavana wa Ohio John Kasich
wakikabiliana vikali katika mchujo wa chama cha Republican jimbo la
Vermont.
Bi Clinton na Bw Sanders pia wanakabiliana vikali katika jimbo la Massachusetts, kaskazini mashariki mwa Marekani.
Matokeo kutoka majimbo yaliyosalia yanatarajiwa kutolea katika saa chache zijazo.
CREDIT: BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment