HATIMAYE
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli imekisikia kilio
cha muda mrefu cha Wananchi ambao walikuwa wakilalamika kupanda kwa
bei ya sukari nchini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari
mchana huu jijini Dar es Salaam Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Sukari
nchini,Henry Semwaza amesema kuanzia sasa kilo moja ya sukari itauzwa
sh. 1800 nchi nzima.
"Serikali, kupitia bodi ya Sukari
Tanzania, inawaarifu wananchi wote kuwa bei ya rejareja ya sukari sasa
itakuwa sh. 1,800 kwa kilo moja. "Amesema Semwaza na kuongeza;
"
Wafanyabiashara wote wanapaswa kuzingatia agizo hili, pamoja na
kuhakikisha kuwa sukari inaendelea kusambazwa na kuuzwa kwa wananchi
bila kuihodhi.
"Maafisa biashara wa mikoa na wilaya watafuatilia
na kusimamia utekelezaji wa agizo kuhusu bei elekezi ya sukari, na
hawatasita kuchukua hatua stahiki za kisheria kwa wale watakaobainika
kupandisha bei ya bidhaa hiyo. "
Tuesday, March 8, 2016
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa tena na maafisa wa polisi. ...
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Na Debora Charles (Mtakwimu) Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini na kuchapisha na kusamba...
-
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya...
-
Mvua kubwa za El-Nino zilizonyesha zimeleta athari maeneo mbalimbali...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment