Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, amemtaka Meya wa Manispaa
ya Kinondoni, Boniphace Jacob, kuacha malumbano ya kisiasa na badala
yake ajikite kufanya kazi.
Onyo
hilo Sadiki limekuja baada ya Meya Jacob kukaririwa akisema manispaa
hiyo ina uwezo wa kukabiliana na uamuzi wa serikali wa kutoa elimu ya
bure bila kuhitaji fedha zinazotolewa na utawala wa Rais John Magufuli.
Halmashauri
ya wilaya ya Kinondoni inaongozwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) ambao ni mwamvuli unaojumuisha wabunge na madiwani kutoka Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha Wananchi (CUF).
Sadiki alisema hahitaji malumbano na kiongozi huyo ambayo hayana tija.
"Mimi sipendi malumbano yasiyo na tija baina ya viongozi," alisema Mkuu wa Mkoa na kuongeza; "unapokataa msaada kama huo wa kupunguza mapungufu katika sekta ya elimu, wanaoathirika ni watu waliowachagua."
Serikali imepanga kutumia Sh. Bilioni 137 kugharamia elimu bure katika miezi sita ya kwanza ya Rais wa tano, Magufuli.
Kiasi
cha Sh. bilioni 18.77 kilitumwa kwenye akaunti za shule za Msingi na
Sekondari za halmashauri zote hapa nchini na vyombo vya usimamizi wa
mitihani kwa kila mwezi wa Januari na Februari, kwa ajili ya wanafunzi
kusoma bure.
Pesa
zilizogawanywa kwenye akaunti za shule za Msingi na Sekondari katika
halmashauri zote ni Sh. bilioni 15.7 kila mwezi na Sh. bilioni 3 kila
mwezi kwenye akaunti vyombo vya usimamizi wa mitihani katika Halmashauri
zote hapa nchini.
Mkuu
wa Mkoa alisema fedha hizo zitapelekwa katika Manispaa zote na ametoa
agizo kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kutumia fedha hizo katika
matumizi yaliyokusudiwa na si vinginevyo.
Sadiki
alisema kwa sababu Rais Magufuli ni kiongozi wa wote, ana haki ya kutoa
kwa wote bila kuzuia wala mipango yake kukataliwa.
"Yule ni mkuu wa nchi, hata kama wanakusanya fedha za kutosha, zipo taratibu za matumizi ya fedha hizo," alisema Sadiki.
Kwa
mujibu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mipango wakati akitoa
taarifa ya kuanza kwa utumaji wa fedha za elimu bure Januari 6, mwaka
huu, walimu wakuu wa shule zote za Msingi na Sekondari katika
halmashauri zote hapa nchini wanatakiwa kuweka wazi matumizi ya fedha
hizo katika mbao za matangazo kwa kila shule, ili kila mzazi aweze kujua
kiasi gani kimetumika.
Sadiki
alikuwa akizungumza wakati akipokea msaada wa ahadi ya ujenzi wa
madarasa 12 katika mkoa wa Dar es Salaam kutoka kwa Wamiliki wa Malori
Tanzaznia(Tatoa), yenye thamani ya Sh. milioni 300.
Mkoa wa Dar es Salaam, alisema Sadiki, una upungufu wa vyumba vya madarasa 7,223, lakini pia uhitaji wa madawati 66,000.
"Yapo
maeneo mengi ya kujenga shule, nawaomba wadau wetu muendelee
kuhamasisha kupata shule nzima kwani shule nzima inahitaji madarasa
kuanzia 22," alisema.
0 comments:
Post a Comment