Juzi,
Diwani wa Kata ya Vijibweni (Chadema), Isaya Mwita alichaguliwa kuwa
umeya akimshinda mpinzani wake Yusuph Yenga (CCM) kwa kura 84 dhidi ya
67.
Akizungumza
jana, Meya Mwita alisema tarehe rasmi ya uchaguzi wa kumpata naibu meya
haijafahamika na kwamba leo atashauriana na uongozi wa jiji na kwamba
mara tu baada ya Sikukuu ya Pasaka ataitisha kikao cha baraza.
Mchakato
wa kumpata naibu meya ni tofauti kwani idadi ya wajumbe watakaopiga ni
ndogo ikilinganishwa na ile ya juzi ambayo madiwani wote na wabunge wote
wa Mkoa wa Dar es Salaam walipigakura.
Mkurugenzi
wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe alisema jana kuwa wajumbe
watakaomchagua naibu meya hawatazidi 25 kutokana na kanuni zilizopo .
Alisema naibu meya atapatikana katika kikao cha kwanza cha Baraza kitakachoongozwa na meya.
Alisema
wajumbe watakaoshiriki kikao hicho ni wabunge wa majimbo, kila
manispaa; Ilala, Temeke na Kinondoni itatoa wajumbe watatu
watakaoteuliwa na mameya wao na Meya wa Jiji atateua watatu.
0 comments:
Post a Comment