WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema agizo lilitolewa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli la kuwataka mawaziri ambao
hawajajaza Tamko la Rasilimali na Madeni wakamilishe kabla ya saa 12
jana jioni limetekelezwa.
Waziri
Mkuu amepokea barua kutoka kwa Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma, Jaji (Mst.) Salome Kaganda ikithibitisha kuwa mawaziri
na naibu mawaziri wote wametekeleza agizo hilo.
“Hadi
kufikia saa 9.30 jana alasiri (Ijumaa, Februari 26, 2016) mawaziri wote
walikuwa wamekamilisha fomu zao za kuzikabidhi katika Ofisi za
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,” alisema Waziri Mkuu.
0 comments:
Post a Comment