MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mjini,
Mchungaji Peter Msigwa na madiwani 14 wanaounda halmashauri ya manispaa ya
Iringa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kesho Desemba 31 watafanya
mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Mwembetogwa mjini hapa kwa lengo
la kuwashukuru wananchi kwa kuwapatia ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba
mwaka huu.
Katika mkutano huo, Mchungaji Msigwa,
Mbunge wa Viti Maalumu Suzan Mgonakulima na Meya wa Manispaa ya Iringa Alex
Kimbe wataonesha muelekeo wa utekelezaji wa majukumu yao katika kipindi cha
miaka mitano ijayo ili kuwaletea wananchi wa jimbo hilo maendeleo.
Mchungaji Msigwa anawaalika wananchi wote wa jimbo hilo, bila kujali itikadi zao kushiriki mkutano huo, na kuukaribisha mwaka mpya pamoja ili kusukuma gurudumu la maendeleo
0 comments:
Post a Comment