METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, August 10, 2015

CCM WAZAZI WA UFISADI NA UKAWA WALEZI

 

 

Akizungumza na wakazi wa iringa mjini waliofika katika viwanja vya mwembetogwa kiongozi mkuu wa chama cha Act amesema ipo haja ya watanzania kujiwekea akiba ya chama hicho kwakuchagua wabunge hata kumi ili kuwatetea watanzania katika bunge lijalo.

Aidha amesema kuwa Ccm ni chama ambacho ni chimbo la mafisadi na chadema ndio walezi hasa wa mafisadi hao ikiwa nisababu iliyofanya Act kutojiunga na chama hicho.

Akielezea juu ya Marais wateule na vyama vyao John Magufuri na Edward Lowasa amesema tofauti yake lowasa ni fisadi na maguri hana tabia ya kuwashughulikia mafisadi hilo likiambatanishwa na matukio kadhaa yaliojitokeza kwenye nchi hii ikiwepo escrow,epa na mengineyo hajawahi kusikika waziri huyo akiongea chchote dhidi ya uchotwaji wa fedha hizo na Lowasa ametuhumiwa kwa muda wa miaka kumi yote ambayo zito akiwa bungeni na safari hii kuonekana akigombea urais.

''huu ni uongo wa kuwageuza watu kama chapati ufike mwisho Mtu akiwa ndani ya ccm fisadi akiingia ndani ya chadema system chadema ni chama kinachobeba madaraka kwasasa kutokana a wimbi la watu na ccm inapagalanyika hivyo wananchi wekeni akiba ya chama kitakachopambana na mafisadi wapya na chama hicho ni ACT, Alisema Zito Kabwe.

Kwaupande wa Chiku Abwao Ambaye ni mbunge aliyepita katika kura ya maoni ndani ya chama hicho yeye alisema kuwa kutokana na vya vilivyounda ukawa vimeamua kukalibisha ufisadi katika chama chao hii ndio sababu iliyopelekea yeye kukihama chama hicho na kujiunga na ACT.

Nae Abuu Majeki amesema kutokana na Mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa kutotimiza ahadi alizo ahidi kipindi cha uchaguzi mwaka 2010 ikiwa hajatimiza hata moja nae ndio sababu kubwa ya yeye kuhamia Act na ametowa shilingi Milioni 1 kwa mwana iringa atakaye elelza kitu alichokifanya mbunge huyo kwa miaka 5 chenye manufaa na wakazi wa iringa na sio wanyama poli.

 

 

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com