Waziri Mkuu Tanzania aonya fitina mbio za Urais CCM
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameonya kuhusiana na fitina kwenye mbio za kuwania Urais ndani ya chama tawala cha mapinduzi nchini humo CCM.
Mizengo Kayanza Pinda amelezea hofu yake juu ya kuwepo kwa fitina zinazofanywa na baadhi ya watu kwa nia ya kuwaharibia wengine katika mchakato wa uteuzi wa wagombea wanaowania kuteuliwa kugombea nafasi ya urais kupitia chama hicho tawala.
Mbali na wasiwasi wake wake huo, Mizengo Pinda ambaye pia ni mmoja wa wanaowania uteuzi huo, amewataka watangaza nia wenzake watakaoshindwa katika kinyang'anyiro hicho kukubali matokeo na kumuunga mkono yeyote atayeibuka mshindi na pia kutambua kuwa 'asiyekubali kushindwa si mshindani'.
Jana alasiri ilikuwa siku ya mwisho ya kurejesha fomu kwa watangaza nia waliochukua fomu za uteuzi wa kiti cha urais ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM. Jumla ya wagombea 42 walichukua fomu huku 38 tu ndio waliofanikiwa kurejesha fomu hizo ambao sifa zao zitapitiwa na hadi kufikia Julai 12 mwezi huu mgombea wa CCM atakuwa amejulikana.. Uchaguzi mkuu nchini Tanzania unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Mrengo wa upinzani kwa upande wake bado unaendelea na mchakato wa kujaribu kusimamisha mgombea mmoja kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA.
0 comments:
Post a Comment