METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, July 2, 2015

ALIYENUSURIKA KIFO TSUNAMI SPORTING LISBON



Sporting Lisbon imemsajili kinda huyu anayejulikana kwa jina la Martunis ambaye alinusurika kufa katika mafuriko ya Tsunami takribani miaka 11 iliyopita.
Sporting Lisbon imemsajili mhanga aliyenusurika katika janga la mafuriko ya Tsunami, Martunis kwenye akademi yao, ikiwa imepita miaka 11 tangu janga hilo kutokea huku likisababisha vifo vya mama yake na kaka zake wawili. Ikumbukwe tu Martunis aliweza kuishi ndani ya dimbwi la maji kwa takribani siku 21.
Martunis, ambaye kwa sasa ana miaka 11, ametambulishwa huko jijini Lisbon akiwa tayari kabisa kutimiza ndoto zake licha ya kupitia misukosuko katika jango hilo mwaka 2004.
Mawimbi hayo makali, yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi katika bahari ya Hindi, yaliua zaidi ya watu 230,000 kutoka mataifa 14 na kusababisha kijana huyo kutengana kabisa na familia yake kwa muda.
 
 
Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo aliguswa mno na stori ya kijana Martunis na kuamua kukutana naye
Kwa sasa, Martunis amejiunga na akademi maarufu ya klabu ya Sporting Lisbon ili kutimiza malengo yake ya kuwa kama Cristiano Ronaldo, na Luis Figo ambaye ameshastaafu.
'Nina furaha kubwa kuwa hapa, klabu hii inanifanya niweze kufikia malengo yangu,' alisema. 'Nina furaha kubwa sana kupata fursa hii. Viva Sporting!
 
 
Martunis akiwa na rais wa FIFA Sepp Blatter
 
 
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com