METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, June 29, 2015

SAMATTA NA ULIMWENGU WOTE WAANZIA BENCHI TP MAZEMBE IKILAZIMISHWA SARE 0-0 NA EL HILAL LUBUMBASHI



Mbwana Samatta (kushoto) na Thomas Ulimwengu wote wameanzia benchi leo Mazembe ikilazimishwa sare ya 0-0 El Hilal mjini Lubumbash

WENYEJI TP Mazembe wamelazimishwa sare ya bila kufungana na El Hilal ya Sudan jioni ya leo katika mchezo wa kwanza wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika, Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi.
Na sare hiyo Mazembe wameshukuru, kwani kipa wao mkongwe Muteba Kidiaba aliokoa mchomo wa hatari dakika za lala salama.
Baada ya kosakosa nyingi, kocha wa Mazembe, Patrice Carteron alimuingiza mshambuliaji Mtanzania, Mbwana Samatta kuchukua nafasi ya Mzambia, Given Singuluma mapema kipindi cha pili ambaye alikwenda kuipa wakati mgumu safu ya ulinzi ya Hilal inayoundwa na wakali kama Nahodha Saif Eldin Masawi, Atir Magor na Muawia Bashir.
Mtanzania mwenzake Samatta, Thomas Ulimwengu aliingia pia baadaye kipindi cha pili, lakini tayari Mazembe walikuwa ‘wamekwishashikwa’ na hakuweza kusaidia kubadilisha matokeo.
Sasa timu zinaanza na pointi moja kila moja, kabla ya mchezo mwingine wa Kundi A kati ya Smouha ya Misri na Moghreb Tetouane ya Morocco baadaye usiku huu mjini Alexandria.
Matokeo ya mechi za awali za Kundi B juzi El Merreikh ya Sudan ilishinda 2-0 nyumbani dhidi ya MC Eulma ya Algeria, wakati jana ES Setif ilifungwa 2-1 na Waalgeria wenzao, USM Alger.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com