Viongozi
wa Afrika masharikiSerikali za Afrika mashariki zimetumia kodi
kuvitahadharisha viwanda vyake kwa upande mmoja na kuwapa motisha
wananuzi wa bidhaa kutoka nje wanaosaidia sekta muhimu kama vile miundo
mbinu,kawi mbali na utekelezwaji wa itifaki ya soko la pamoja.
Katika
mapendekezo ya bajeti yaliosomwa siku ya alhamisi Kenya, Uganda Rwanda
na Tanzania zimepunguza kodi za bidhaa zinaozoagizwa kutoka nje kwa
sekta muhimu kama vile kawi,mawasiliano na miundo mbinu.BBC
Kulingana
na gazeti la the east African nchini Kenya, shinikizo la kuimarisha
miundo mbinu, kupunguza gharama ya kufanya biashara na kuongeza
mtiririko wa mapato kutoka kwa mafuta na gesi iliogunduliwa katika eneo
la Afrika mashariki umeyafanya mataifa manne ya eneo hili kushusha
masharti ya sera za kodi ili kurahisisha biashara na majirani zao pamoja
na mataifa ya kigeni.
Rwanda imepunguza kodi katika magari yanayoagizwa kutoka nje hususan matinga tinga,malori pamoja na mabasi ya uchukuzi.
Tanzania
kwa upande wake imechukua mkondo kama huo na kupunguza kodi ya kuagiza
bidhaa kutoka nje kutoka asilimia 25 hadi 10 miongoni mwa mabasi
yanayobeba abiria 25 kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Uwiano wa kikanda unalenga kurahisisha biashara na kuzuia hasara inayokumba kampuni zinazofanya biashara katika eneo hili.
Hatahivyo,wafanyibiashara
katika mataifa kama vile Rwanda na Uganda wanalazimika kulipia hasara
inayotokana na masharti ya kibiashara yaliowekwa na wasanifu.
Ili kuondoa matatizo hayo Kenya
imetangaza kuwa inapunguza masharti kadhaa ya kibiashara kupitia kuondoa
forodha ya usalama katika uagizaji wa sukari ya viwanda na unga na
ngano.
Uganda nayo imechukua mkondo huo kwa
kuondoa forodha yake ya usalama kwa bidhaa na kuanzisha mtindo wa kulipa
unaojulikana ambao unalenga kuleta uwiano.
0 comments:
Post a Comment