METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, December 5, 2023

ZAIDI YA WAJASIRIAMALI 300 KUSHIRIKI MAONESHO YA NGUVU KAZI/ JUA KALI NCHINI BURUNDI

Na; Mwandishi Wetu – Bujumbura, BURUNDI 

WAJASIRIAMALI zaidi ya 300 kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania kushiriki maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayofanyika Bujumbura, Burundi kuanzia tarehe 5 hadi 15 Desemba, 2023.

Maonesho hayo yanafanyika katika Viwanja vya Cercle Hyppique (Golf Course), Bujumbura yakiongozwa na kauli mbiu isemayo ‘Kuunganisha Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Afrika Mashariki kufanya biashara katika eneo la Jumuiya ya Afrika Mashariki’.

MWISHO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com