METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, December 13, 2023

RAIS SAMIA ASIHUSISHWE KUAHIRISHWA MAADHIMISHO MIAKA 30 CWT - PROF. NDALICHAKO


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema taarifa zinazo sambazwa kwenye mitandao ya kijamii juu ya kuhairishwa kwa maadhimisho ya miaka 30 ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) hakuhusiani na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhairisha kushiriki Maadhimisho hayo.
 
Maadhimisho hayo yalikuwa yafanyike Jijini Mwanza Desemba 16, 2023 ambapo Mhe. Rais aliridhia mwaliko wa CWT Novemba 14, 2023 kuwa Mgeni rasmi na baadae CWT waliomba kubadili tarehe ya maadhimisho ifanyika Desemba 13 badala ya tarehe aliyoridhia Mhe. Rais.

Prof. Ndalichacho amebainisha hayo Desemba 12, 2023 Jijini Dar es salaam ambapo amesema Mhe. Rais alielekeza wataarifiwe tarehe waliyoibadilii atakuwa na jukumu linguine licha CWT kuendelea na maandalizi na kubadilisha hadi  Desemba 16, 2023.

Aidha, Mhe. Ndalichako amewahakikishia walimu nchini kuwa serikali ya awamu ya Sita inatambua na kuthamini mchango wao na itaendelea kushirikiana na Wafanyakazi wote wakiwemo walimu ambao wanafanya kazi kubwa ya kuwalea na kuwajengea ujuzi watoto kwa ajili ya kujenga Taifa na ustawi kwa watanzania.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com