Na Saida Issa,Dodoma
MBUNGE wa Mvumi Livingstone Lusinde ameipongeza serikali kwa kuwaza uwekezaji katika eneo la Bandari ya Dar es salaam huku akitaja faida za uwekezaji huo ikiwemo kuongezeka kwa fursa za ajira,kupungua kwa urasimu wa kuchelewa kwa mizigo na kuongeza mapato ya bandari kutoka trilioni 7.7 hadi kufikia Ttrilioni zaidi ya 20.
Mbunge huyo ameyaeleza hayo Jijini Dodoma alipokuwa akitolea ufafanuzi kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA kuhusu Uwekezaji wa bandari ya Dar es salaam.
Kutokana na hilo amekemea kauli zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa ambazo zipotosha na kuleta ubaguzi katika Taifa.
"Nia ya Mheshimiwa Rais kukutana na kuzungumza na viongozi wa vyama vyote na kuruhusu wafanye mikutano ni kuleta utangamano wa Taifa,Mimi kama Mjumbe wa NEC nampongeza sana Mheshimiwa Rais kwani ameruhusu Hoja zijibiwe Kwa Hoja,hajaruhusu ubaguzi Wala mitifuano isiyo na sababu,"amesema kibajaji.
Alisema kuwa Rais anapaswa kuongoza Taifa lote kwa pamoja na sio Kwa mipaka kwani na Rais kuitolea maamuzi bandari ya Dar es salama ni suala la kawaida Kutokana na majukumu yake.
"Huu ubaguzi anaoufanya na Mwenyekiti wa CHADEMA sio suala la kuliacha lipite amekuwa akisema kuwa Rais anatoka Zanzibar na Waziri wa Ujenzi na uchukuzi anatoka Zanzibar hii sio Leo tu kwani tumekuwa na Waziri wa fedha Saada Mkuya wakati wa Jakaya Kikwete na amefanya kazi vizuri na mbarawa hakuteuliwa tu na Samia kwani amekuwa Waziri tangu enzi za Kikwete,"alisema kibajaji.
Kadhalika alimpongeza Rais Samia kwa uamuzi wake kuridhia bunge lijadili na kupitisha maazimio mbalimbali yatakayoletwa na serikali katika uwekezaji jambo ambalo linafanyika kwa mara ya kwanza.
0 comments:
Post a Comment