METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, May 23, 2023

SERIKALI INAENDELEA NA UKARABATI WA MAGEREZA NCHINI.


Na Saida Issa, Dodoma

SERIKALI imesema kuwa mpango wa ukarabati wamagereza unaendelea kuanzia mwaka Jana pia mwaka kulingana na upatikanaji wa fedha.

Hayo ameyaeleza Bungeni Jijini Dodoma Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Jumanne Sagini alipokuwa akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Vitimaalumu Mkoa wa Pwani Subiri Mgalu alipouliza kuwa Serikali inasema Nini juu ya nyumba chakafu zilizopo katika gereza la dimani na je Kutokana na changamoto ya uchakavu wa miundombinu inafanana na gereza la kigongoni bagamoyo bado kunanyumba chakavu ni lini Serikali itawajengea nyumba kama inavyofanya kwa majeshi mengine?

Naibu Waziri amesema kuwa Serikali itapelekea fedha za ukarabati katika gereza na mkuu wa gereza pamoja na Uongozi wake wataangalia niwapi kunatatizo kubwa zaidi na wanalipa kipaumbele na hawataagiza nini kianziwe kukarabatiwa.

"Fedha hizo tutazipeleka moja Kwa moja Kwa mkuu wa gereza nayeye ndiye atakayeamua kwa kuangalia kipi ambacho kinahitajika kuanza kukarabatiwa kama gereza Lina hali mbaya zaidi basi wataanza na gereza kama nyumba inahali mbaya zaidi wataanza ma nyumba,

Kwaiyo uhuru tunawaachia wao lakini kuhusu ukarabati wa gereza la bagamoyo nikuhakikishie kuwa mpango wetu wa kukarabati magereza unaenda sambamba kwa Nchi nzima na tumeanza mwaka Jana na mwaka huu tunaenda na pia mwaka kesho tunaendelea na ukarabati wa magereza,"amesema.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com