Na Saida Issa, Dodoma
SERIKALI imesema kuwa ipo kwenye maandalizi ya kujenga barabara ya Igawa Songwe Tunduru (km 218) pamoja na barabara ya mchepuo ya Mlima wa Nyoka (Uyole) hadi Uwanja wa Ndege wa Songwe (Uyole Songwe Bypass) yenye urefu wa kilometa 48.9 kwa utaratibu wa EPC+F (Engineering, Procurement, Construction plus Finance).
Hayo ameyaeleza Naibu Waziri Ujenzi na uchukuzi Mhandisi Geodfref Kasekenya alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbeya Vijijini Oran Manase Njeza, alipouliza Je, ni lini Serikai itajenga barabara ya Mchepuko ya Mlima Nyoka (Uyole) hadi Uwanja wa Ndege wa Songwe ili kuondoa msongamano na ajali.
Naibu Waziri huyo amesema kuwa Hadi sasa Mkandarasi ameshapatikana na mkataba wa ujenzi utakuwa umesainiwa kabla ya mwisho wa Mwezi Juni, 2023.
0 comments:
Post a Comment