Na
Dotto Mwaibale, Singida
BARAZA
Kuu La Waislam Tanzania (BAKWATA) , Mkoa wa Singida limelaani vikali na kupinga
tabia ya baadhi ya watu ya kumdhalilisha Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi Bin Ally.
Akizungimza
kwa niaba ya Bakwata na waislamu Sheikh wa Mkoa wa Singida Issa Nassoro Issa
alisema jambo hilo halivumiliki hata kidogo na kuwataka waliofanya hivyo kuacha
mara moja, kwani Mufti ni kiongozi Mkuu wa Dini ya Kiislamu nchini na kama
kulikuwa na jambo lolote dhidi yake wangeenda kumuona badala ya kukimbilia
kwenye vyombo vya habari.
Hatuta
kubali kuona watu wote wanaoingilia utendaji kazi wa Bakwata na kumdhalilisha
Mufti kwa kauli za kejeli kama ilivyotokea hivi karibuni ambapo Muadhiri mmoja
akimtaka ajipime.
“
Jambo hilo sio nzuri hata kidogo ebu tujipime mapema mwaka jana Mufti wa
Tanzania alikuwa Misri ambapo chuo kimoja kikubwa kilimtunuku Tuzo ya heshima
ambapo pia alifanya mambo mengi kwa ajili ya waislam halikadharika na Kenya pia
walimtunuku tuzo kama hiyo sasa kiongozi wa namna hii kwanini adhalilishwe”
alisema Sheikh Nassoro.
Alisema
kuambiwa Mufti ajipe Bakwata Singida inaona wanaosema hivyo wamelenga kuleta
machafuko hapa nchini na kutaka kumdhalilisha Mufti na kumshusha hadhi yake.
Alisema
kitendo hicho wanakipinga kwa nguvu zao zote kwani Mufti anatosha kuwa kiongozi
na ndio maana dunia nzima inamtambua na wametoa angalizo kuwa sio kila mtu
anaweza kuwa msemaji na kuwa
wapoviongozi wenye mamlaka ya kuzungumza kwa niaba ya waislam.
Nassoro
alisema ifike wakati wa kuchunga mipaka ya kinidhamu waliopewa wanadamu hivyo
hawatapenda kuona watu wachache wakijitokeza na kuanza kushambulia masheikh na
Mufti.
Sheikh Nassoro ametumia nafasi hiyo kuiomba Serikali iwaangalie kwa kina watu wanaotumia nafasi ambazo sio zao kwa kutaka kuchafua hali ya utulivu na amani uliopo katika nchi yetu.
0 comments:
Post a Comment