METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, December 19, 2022

KAWAIDA AWAONYA WANAOBEZA ZIARA ZA RAIS DKT.SAMIA

Mwenyekiti wa umoja wa vijana  wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM) Ndg.Mohamed Ali Kawaida akivalishwa Skafu mara baada ya kuwasili mkoani Singida 18 Disemba 2022. 
Mwenyekiti wa umoja wa vijana  wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM) Ndg.Mohamed Ali Kawaida akizungumza katika hafla ya mapokezi ya viongozi wakuu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM) mkoani singida 18 Disemba 2022.

makamu Mwenyekiti wa umoja wa vijana  wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM )Ndg. Rehema Sombi akizungumza katika hafla ya mapokezi ya viongozi wakuu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM) mkoani singida 18 Disemba 2022.

Mwenyekiti wa umoja wa vijana  wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM) Ndg.Mohamed Ali Kawaida akiwa katika picha ya pamoja na makamu Mwenyekiti (UVCCM) Taifa Ndg. Rehema Sombi, katibu mkuu (UVCCM) Taifa Ndg. Kenan Kihongosi na viongozi wengine wa (UVCCM) katika hafla ya mapokezi ya viongozi wakuu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM) mkoani singida 18 Disemba 2022.

Mwenyekiti wa umoja wa vijana  wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM) Ndg.Mohamed Ali Kawaida akiwa katika picha ya pamoja na makamu Mwenyekiti (UVCCM) Taifa Ndg. Rehema Sombi na katibu mkuu (UVCCM) Taifa Ndg. Kenan Kihongosi katika hafla ya mapokezi ya viongozi wakuu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM) mkoani singida 18 Disemba 2022.


Mapokezi ya viongozi wakuu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM) mkoani singida 18 Disemba 2022.

Mwenyekiti wa umoja wa vijana  wa chama cha mapinduzi wilaya ya Dodoma Mjini Ndg.Shabani Shabani  akiwa katika picha ya pamoja na katibu wa  umoja wa vijana  wa chama cha mapinduzi wilaya ya Dodoma Mjini Ndg.Isack Ngongi katika hafla ya mapokezi ya viongozi wakuu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM) mkoani singida 18 Disemba 2022.

Na Rasuli Kidindi, Juma Wage Singida.

Mwenyekiti wa umoja wa vijana  wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM) Ndg.Mohamed Ali Kawaida amewaonya wanaobeza ziara zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan nje ya nchi huku akisema ziara hizo ni zakutafuta fursa mbalimbali ikiwemo uwekezaji na sio za kutembea.

Ndg. Mohamedi Ali kawaida ameyasema hayo Disemba 18 mkoani Singida katika hafla ya mapokezi ya viongozi wakuu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM) mkoani humo akiwa ameongozana na makamu mwenyeki (UVCCM) Taifa Ndg. Rehema Sombi na katibu mkuu (UVCCM) Taifa Ndg. Kenan Kihongosi ambapo amesema jumuiya hiyo haitawavumilia wanaobeza ziara mbalimbali za  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Aidha Ndg. Mohamed Ali Kawaida amesema wataendeleza na kuulinda umoja wa vijana kwa manufaa ya chama pamoja na maendeleo ya nchi.

“ Umoja wetu wa vijana tutauendeleza na kuulinda na yoyote atakayezingua tutamchapa” alisema Kawaida

Kwa upande wake makamu Mwenyekiti wa umoja wa vijana  wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM) Ndg. Rehema Sombi ameahidi kufanya kazi kwa waledi na kujituma ili kuwalipa imani vijana kwa kuwaamini na kuwachagua kuwa viongozi wao huku akisisitiza uchaguzi umekwisha sasa ni muda wa kufanya kazi na kuacha makundi.

Pia Ndg. Rehema Sombi ametumia fursa hiyo kuwaasa vijana kujiepiusha na matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na kutumia vizuri mitandao ya kijamii.

Awali naye katibu mkuu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM)  Ndg. Kenan Kihongosi akatumia fursa hiyo kuwataka vijana kuacha chuki, fitna na majungu na kujikita katika kufanya kazi .

Pamoja na mambo mengine vilevile Ndg. Kenan Kihongosi amewasihi vijana kukilinda chama na kuyasemea mambo mazuri yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com