METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, November 26, 2022

DKT. KAPOLOGWE AELEKEZA HUDUMA ZIANZE KUTOLEWA KITUO CHA AFYA NTUNTU – IKUNGU

 

Timu ya Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa jamii kutoka ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  ikiongozwa na Mkurugenzi Dkt. Ntui Kapologwe ikiwa katika picha ya Pamoja baada ya Kukagua Ujenzi wa Kituo cha Afya Ntuntu kilichopo Ikungi - Mapema hii leo Novemba 26 2022.


Miongoni mwa majengo yaliokamilika ambayo Dkt. Kapologwe aliyoyatembelea na kuridhishwa  nayo.

Ujenzi unaedelea kituo cha afya Ntuntu Ikungi Singida.

Ukaguzi wa majengo ya kituo cha afya Ntuntu ukiendelea kwenye ziara ya Dkt. Ntui Kapologwe.

Mkurugenzi wa huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais   Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI) Dkt. Ntuli Kapologwe ameielekeza Timu ya Huduma ya afya Wilaya ya Ikungi Kwa kushirikiana na ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida  kuanza kutoa Huduma kwa wananchi katika kituo cha afya cha Ntuntu.

Mkurugenzi Hugo wa Huduma za afya, Lishe na Ustawi wa Jamii kutoka OR-TAMISEMI ametoa maelekezo hayo kufuatia ziara yake  ya kutembelea Kituo Cha Afya Ntuntu kilichopo Ikungi mkoani Singida kujionea hatua mbalimbali za ujenzi wa Kituo hicho .

Dkt. Kapologwe akiwa pamoja na timu  kutoka ofisi hiyo wakiongozana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida na Timu yake (RHMT) wametembelea kujionea majengo mbalimbali ya kituo hicho ambapo lengo ni kuona ujenzi unavyoendelea.

Dkt. Kapologwe  ameipongeza timu nzima ya usimamizi wa ujenzi wa Kituo hicho cha Afya kwa ukamilishaji mzuri wa majengo 3 ya awamu ya kwanza (Jengo la Wagonjwa wa Nje OPD, Jengo la Maabara na Kichomea Taka) ambao mpaka sasa umekamilika kwa asilimia 99% .

Mkurugenzi huyo sambamba na pongezi hizo katika usimamizi wa ujenzi wa kituo hicho cha afya alitoa maelekezo  ya huduma zianze kutolewa kwa wananchi ifikapo jamatatu ya Novemba 28.

Serilikali ipo kwenye hatua za mwisho za uletaji was vifaa Tina mbalimbali katika kituo cha afya hichi hivyo wananchi waanze kupata Huduma kuanzia jumatatu ya tarehe ya wiki ijayo" alisema Dkt.  Kapologwe.

Aidha Katika majengo mengine  matatu ya awamu  ya pili ambayo Mkurugenzi wa OR-TAMISEMI  Dkt. Ntui Kapologwe ni pamoja na  Jengo la Wodi ya Wazazi (Maternity), Jengo la Upasuaji (Theatre) na Jengo la Kufulia (Laundry)  ambapo ujenzi huyo umefikia zaidi ya asilimia 60%  na kutoa maelekezo kuwa Kasi ya ujenzi huo  iongezeke hadi kufikia Disemba 30 Majengo hayo yawe yamekamilika ili kufikia malengo ya Serikali ya kupeleka huduma kwa wananchi wa Ikungi hasa kata ya Ntuntu.

Ujenzi wa Vituo vya afya ni moja ya mkakati na kipaumbele cha serikali ya awamu ya sita chini ya Raid Samia  kuhakikisha kuwa wananchi wanapata Huduma za afya katika maeneo ya karibu na makazi yako na Wilaya ya Ikungi imeendelea kutekeleza maelekezo ya Serikali katika sekta ya Afya kwa maslahi ya wananchi.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com