METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, September 28, 2022

UTEUZI WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA KWA WAGOMBEA WA NAFASI ZA UENYEKITI WA CCM WILAYA

                                           


TAARIFA KWA UMMA


Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC) imekutana chini na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa White House Makao Makuu, Jijini Dodoma Jumanne tarehe 27 Septemba, 2022.

Pamoja na mambo mengine Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imefanya uteuzi wa majina ya wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa CCM wilaya kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2022 ibara ya 82(1) ambapo mikutano mikuu ya wilaya itafanyika kote nchini kuanzia tarehe   01 -02 Oktoba, 2022.                

Aidha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) imeongeza muda wa kuchukua na kurejesha fomu kwa nafasi zote za Halmashauri Kuu ya Taifa ambapo zoezi hilo la kuchukua na kurejesha fomu litaanza tarehe 1-5 Oktoba, 2022 kwenye Ofisi za mikoa, Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu Dar es Salaam na Makao Makuu ya CCM Dodoma.

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
Itikadi na Uenezi
27 Septemba, 2022



Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com