Maganga Gwensaga Kongwa, Dodoma
Mkurugenzi wa Afya kutoka shirika USAID Nchini Bi. Anne Murphy ameonyesha kuridhishwa na kazi ya utoaji wa chanjo ya Uviko-19 na shughuli nyingine zinafadhiliwa na shirika Hilo Wilayani Kongwa.
Pongezi hizo amezitoa Sept 13, 2022 muda mfupi baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa zoezi la utoaji wa chanjo ya uviko-19 Katika Wilaya ya Kongwa ukiwa ni mmoja Kati ya mradi unayofadhiliwa na shirika Hilo.
Mbali na hilo, Mkurugenzi huyo alipongeza ushirikiano mkubwa baina ya Viongozi wa Wilaya akisema kuwa amefurahishwa zaidi na umoja huyo.
“Tumefurahishwa sana na ushirikiano wenu na bidii Katika kazi, tuna mategemeo makubwa zaidi na nyie nasi tunaahidi kuendelea kushirikiana nanyi.” Alisema Bi. Anne
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Remidius Mwema aliwashukuru USAID kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiutoa na kuahidi kuendelea kushirikiana na wadau kufanikisha malengo Katika sekta ya Afya.
“Niwahakikishie Serikali, inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kushirikiana na USAID Katika utekelezaji wa afua mbalimbali za sekta ya Afya Wilayani hapa.” Alisema Mwema
Akiwa Wilayani humo Bi. Anne alitembelea kituo Cha Afya Cha Ugogoni na kushuhudia zoezi la utolewaji wa chanjo ya uviko likiendelea.
Tangu mwaka 2019 hadi sasa Serikali imetoa jumla ya shilingi Bilioni 6.23 kwa Wilaya ya Kongwa na kuwezesha ujenzi wa Vituo vipya 5 vya Afya (Chamkoroma, Pandambili, Chitego,Songambele na Sejeli) pamoja na Upanuzi wa Vituo ya Afya Viwili ( Kibaigwa na Mkoka) na umaliziaji wa Zahanati 9.
Jitihada za Serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za Afya na kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hii.
Kwa kipindi kirefu sasa USAID wamekuwa ni wadau muhimu katika kufanikisha utekelezaji wa Miradi mbalimbali katika Sekta ya Afya hapa nchini ikiwa ni pamoja na Wilaya ya Kongwa.
Pamoja na mambo mengine, USAID kupitia JHPIEGO wamekuwa wadau muhimu kwa kushirikiana na Serikali katika kufanikisha huduma za Chanjo za Kawaida & UVIKO-19
Wilayani humo.
0 comments:
Post a Comment