METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, August 27, 2022

WASIMAMIZI WA SENSA SINGIDA WATAKIWA KUWAFUATILIA MAKARANI KUZIFIKIA KAYA AMBAZO HAZIJAHESABIWA

 


Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akiwa ameambatana na mkuu wa wilaya ya Ikungi Jerry Muro akipokea maelezo ya jinsi zoezi la sensa linavyoendelea katika halmashauri ya ikungi mapema hii leo

RC Serukamba na DED wa Ikungi Justice kijanzi akishuhudia uhalisia na ugumu wa zoezi la sensa wakitembea kwa miguu mtaa kwa mtaa katika halmashauri ya Ikungi

RC Serukamba akizungumza na Wasimamizi wa Makarani Wa Sensa halmashauri ya Ikungi kabla ya kuaanza kutembelea kaya kwa kaya kukagua zoezi hilo.



Karani wa sensa Skovia Deus kutoka ofisi ya Takwimu ikungi akitoa  maelezo kwa mkuu wa mkoa Peter Serukamba  ya kaya alizozifikia hadi sasa

Karani katika ubora wake akiwajibika 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ikungi Justice Kijazi akitoa taarifa ya kaya zilizokwisha hesabiwa hadi kufikia jana agosti 26 ambapo ni kaya 51,109 Sawa na asilimia 85.3% 59,911

Mzee Rashid mkazi wa Ikungi akisalimiana na RC Serukamba baada ya kushiriki zoezi la sensa

Na Hamis Hussein - Singida

Mkuu wa mkoa wa Singida Peter Serukamba amewataka wasimamizi wa makarani wa sensa waliomaliza kufanya madodoso katika maeneo waliopangiwa kuwahamisha kwenda kuongeza nguvu maeneo mengine ambayo bado zoezi la sense halijawafikia.

RC Serukamba amesema hayo baada ya kukagua zoezi la sensa kwenye kaya za Singida Mjini, Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi na Itigi Mkoani humo ambapo amesisitiza kamati za sensa za kila halmashauri kuongeza kasi ya kuzifikia kaya hadi kufikia jumatatu ya agosti 29 ili kufanikisha zoezi hili.

“Zoezi linaenda vizuri sana, na utaona tumeshaandikisha watu wengi sana Halmashauri zingine zimefikia asilimia 80% ukiacha halmashauri ya itigi ambayo inachangamaoto ya geografia yao ya umbali hivyo kuwalazimu makarani kutembea umbali mrefu lakini tumeweza kuwajazia mafuta kwenye pikipiki ili wazifikie kaya nyingi”. Alisema RC Serukamba.

Ameongeza kuwa ili kuongeza kasi hiyo ya kuandikisha kaya nyingi Zaidi wasimamizi wa sensa pamoja na waratibu wawe karibu kuwafuatilia makarani ili watakapomaliza maeneo waliopangiwa wahamishiwe kwenye kaya zingime ambazo hazijafikiwa.

“Msisitizo wangu nimewambia ni kuwa wale makarani waliomaliza zile kaya walizopangiwa  wahamishiwe kwenye kaya zingine nimewaambia maafisa takwimu wa wilaya kufanya hilo na tumeona kote nilikopita wapo makarani ambao wamemaliza kaya walizopangiwa na wamepewa kaya zingine nia yetu ni kutaka tusaidiane ili tuweze kumaliza vizuri”. Aliongeza RC Serukamba.

Mratibu wa Sensa mkoa wa Singida Naing’oya Kipuyo amesema kuwa kuletwa kwa vifaa vya kuchajia vishikwambi pamoja na kutumia bakaa ya fedha kwaajili ya kuwawekea makarani mafuta ili kuzifikia kaya zilizopo mbali  imeongeza kasi ya uandikishaji wa kaya ukilinganishwa na hapo awali ambapo karani alikuwa analazimika kuacha zoezi hilo kutokana na umbali na vishikwambi kukosa chaji.

“Serikali imetoa ruhusu ya kutumia bakaa ya fedha kurahisisha zoezi hili waratibu wa sensa wa Wilaya ama kwenye Halmashauri wamekuwa wakikodisha jenereta na pikipiki na kuweka mafuta  kuhakikisha zoezi linamalizika katika siku saba ambazo zimepagwa tofauti na hapo awali ambapo makarani hasa wa maeneo ya pembezoni  ilikuwa ikifika saa sita mchana chaji imeisha na kusimamisha zoezi anaenda kulala mpaka Kesho” alisema Kipuyo.

Katika Halmashauri ya Ikungi Mkurugenzi Justice Kijazi amesema kuwa kufikia jana agosti 26 tayari kaya 51,109 Sawa na asilimia 85.3% 59,911 lakini akitaja changamoto ambazo zimejitokeza kwenye zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kuzima na kuharibika kwa vishikwambi, baadhi ya wananchi kugoma kuhesabiwa, pamoja na mwingiliano wa mipaka kati ya Wilaya na wilaya, Kata na kata na kusema kuwa changamoto hizo zimeshapatiwa ufumbuzi.

Kwa upande wake mratibu wa Sensa wa Halmashauri ya Itigi Sophia Selemani amesema katika kuzitatua changamoto zinapelekea zoezi hilo kususa  tayari wamepokea Vitunza Chaji Power Bank 80 huku akiomba kuongezewa kwa Vitunza Chaji 40 ili kukidhi mahitaji na kuongeza licha changamoto ya Jeografia wanaokumbana nayo lakini kufikia jana Agosti 26 tayari wameshazifikia kaya 20,694 sawa 71.4% kati ya kaya 28,992.

 


 

 

 

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com