METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, August 18, 2022

TFRA, CRDB yatoa mafunzo kwa mawakala wa mbolea ya ruzuku


Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kwa kushirikiana na kampuni ya bizytech ambaye ni mwakilishi wa CRDB wametoa  mafunzo ya jinsi ya kutumia mfumo wa kidigital wa mbolea kwa wafanyakazi na mawakala 18 wa one acre fund  mkoani Iringa.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Kaimu Meneja wa Uingizaji na Uuzaji Mbolea Nje ya Nchi, Louis Kasera alisema mafunzo hayo yana lengo la kuwajengea uwezo mawakala na wauzaji wa mbolea juu ya namna ya kutumia mfumo wa mbolea ya ruzuku.

Baada ya mafunzo hayo,  Kasera amewataka mawakala hao kuanza kufanya mauzo ya mbolea za ruzuku kwa wakulima ili kutimiza ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuanza kutekeleza mpango huo wa kutoa ruzuku kwa wakulima msimu huu wa kilimo. 

Mafunzo hayo ya siku moja yalifanyika katika ukumbi wa wakala wa mbolea wa One Acre Fund Mkoani Iringa jana tarehe 17 Agosti, 2022.

Mafunzo hayo yanaendelea kutolewa nchi nzima kwa mawakala na wauzaji wote wa mbolea ambapo Kesho mafinzo hayo yatafanyika Makambako mkoani Njombe na Tabora.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com