METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, July 12, 2022

MSITUMIE MICHEZO KWA MASLAHI YENU BINAFSI RC-TABORA

    

Na Lucas Raphael,Tabora

Kamati ya maandalizi ya michezo ya Umitashumta inayotarajiwa kufanyika kitaifa mkoani Tabora mwaka huu imetakiwa kuimarisha umoja na mshikamano bila kutanguliza maslahi binafsi mbele.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Batilda Buriani katika ufunguzi wa mashindano ya michezo ya UMITASHUMTA ngazi ya mkoa katika viwanja vya Chuo cha Ualimu mkoani Tabora.

Alisema kwamba kamati hiyo inatakiwa kuhakikisha maandalizi yanafanikiwa ni muhimu kutanguliza uzalendo mbele na kujitoa kufanya hivyo kunajenga furaha kwa jumuiya nzima ya michezo

Alisema michezo hiyo itakayofanyika mkoani Tabora kitaifa mapema mwaka huu itaisaidia kuutangaza mkoa huo kwa kutoa hamasa ya kutosha kwa wananchi  ili waweze  kushiriki kwenye mashindano na kuushangilia mkoa mwenyeji kwenye  mashindono hayo

Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa wa Tabora aliwataka waandaji hao Kutoa ushirikiano wa kutosha kwenye timu ya maandalizi ya Michezo Taifa katika masuala yote ya Mapokezi ya wanamichezo, walimu na Viongozi mbalimbali kutoka katika Mikoa yote Tanzania.

“Kuwapanga vizuri wafanyabiashara mbalimbali katika maeneo ya kufanyia biashara kwenye kituo cha mashindano ili kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wanamichezo na hivyo kuboresha shughuli za Michezo kitaifa” alisema Batilda Buriani.

Awali Afisa Elimu Mkoa wa Tabora Juma  Kaponda alimweleza Mkuu wa Mkoa kwamba jumla ya wanafunzi na walimu 1,104 wanashirikia michezo hiyo ngazi kwa ajili ya maandalizi ya kupata timu itakayo wakilisha  mkoa kwenye mashindano hayo.

Alisema kwamba mkoa unaendela kusimamia Ukarabati wa Viwanja vitakavyotumika kitaifa katika shule za Sekondari ya Wavulana Tabora na Shule ya Wasichana ya Tabora.

Aliongeza kuwa tayari wamepokea kiasi cha shilingi 800,000,000 toka Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa ajili ya kuzifanya shule hizo mbili kuwa Kituo cha Michezo ya Kitaifa.

Alisema kwamba lengo likiwa ni kuendelea kusimamia Ukarabati wa Majengo katika shule hizo mbili.

Mkoa wa tabora katika mashindano ya Umitashumta kitaifa mwaka 2021 ilishika nafasi ya saba.

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com