METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, April 30, 2022

RC MAKALLA: VYANZO VYA MAJANGA MENGI YA MOTO KWENYE MASOKO NI UZEMBE




Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo April 29 amefanya kikao Cha pamoja baina yake, Viongozi wa Masoko na Jeshi la Zimamoto na uokoaji kwa lengo la kutoa Elimu ya udhibiti wa Majanga ya Moto kwenye masoko ya Mkoa huo.


Uamuzi wa RC Makalla kuhitisha kikao hicho ni Kufuatia kuungua kwa baadhi ya Masoko ndani ya Muda ambapo ripoti za Kamati zinazoundwa kuchunguza zinaonyesha kuwa chanzo ni Uzembe wa watu kujiunganishia umeme kiholela na kinamama kuhinjika maharage kwenye majikoni usiku ili asubuhi wakute yameiva.

Kutokana na changamoto hiyo RC Makalla ameelekeza kila soko kuwa Vifaa vya kudhibiti moto na fundi wa umeme anaetambuliwa na TANESCO.

Aidha RC Makalla ameelekeza Jeshi la Zimamoto na uokoaji kuandaa ratiba ya kupita kila soko la Mkoa huo na kutoa Elimu ya kujikinga na majanga ya Moto.

Kuhusu changamoto ya uchakavu wa Masoko iliyolalamikiwa na Viongozi wa masoko, RC Makalla ameelekeza Kila Halmashauri kupitia Wakurugenzi na Maafisa biashara kuboresha Masoko, Barabara, Maji, Vyoo na kununua vizimia Moto.

Kwa upande wao Viongozi wa masoko Wamemshukuru RC Makalla kwa kuona tatizo lililopo na kuamua kuhitisha kikao Cha kupatia majibu changamoto ya Masoko kuuungua ambapo wameeleza kuwa kwa miaka mingi haijawahi kutokea kiongozi akahitisha kikao Kama hicho Cha kutoa Elimu ya kujikinga na majanga ya Moto hivyo kitendo alichofanya kimewapa matumaini makubwa.

Itakumbukwa kuwa hivi karibuni kumeibuka matukio ya kuungua moto kwa baadhi ya Masoko ikiwemo 
Soko la Kariakoo, Coca-cola, Karume, Mbagala na Soko la mchikichini.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com