Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania Dkt.Efrem Njau amesema kuwa Mradi wa kutoa msaada wa kupunguza sumu za Viuatilifu zenye madhara makubwa kwa afya ya binadamu na mazingira umekuwa ni mradi wa mfano kwani umemaliza malengo yote saba (7) yaliko kwenye mkataba ndani ya muda uliopangwa na utakwenda kukomboa Wdau wa Viuatilifu na watanzania Kwa Ujumla
Dkt Njau ameyasema hayo hivi leo Aprili 13/2022 hapa jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa kisera wa kupokea taarifa muhimu ya utafiti uliofanywa na watatifi kutoka mamlaka ya afya ya Mimea na Viuatilifu uliohudhuriwa na wadau mbalimbali ikiwemo Mwakilishi wa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani, Ndugu, Diomedes Kalisa,Mwenyekiti wa umoja wa wafanyabiashara wa Viuatilifu (croplife Tanzania), Ndugu, Harish Dhutia,Wawakilishi kutoka Mashirika yasiyo na Kiserikali,wadau wa Viuatilifu kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania,Maofisa wa Serikali kutoka Taasisi na Mashirika mbalimbali, Wataalamu wa TPHPA na Viongozi
Ambapo amesema kuwa Mamlaka ya afya ya Mimea na Viuatilifu kwa kushirikiana na shirika la Chakula duniani kwa ufadhili wa Serikali ya umoja wa Ulaya tumetekeleza mradi wa kufanya tathmini ya Viuatilifu vinavyotumika hapa nchi kama vinakidhi vigezo vya kimataifa, mradi ujulikanao kama Support for Reducing Risks of Highly Hazardous Pesticides and promoting safer alternatives in the United Republic of Tanzania (URT) Phase ya tatu (MEA3)” (Mradi wa kutoa msaada wa kupunguza sumu za Viuatilifu zenye madhara makubwa kwa afya ya binadamu na mazingira).
Aidha ameongeza kuwa Mamlaka iliingia Mkataba (letter of Agreement) wa kutekeleza mradi huu tarehe 20 July 2021, Katika mkataba huo jumla ya malengo saba (7) yametekelezwa yakiwemo:-
1. To review and update current HHPs list according to pre-defined criteria as set by the FAO/WHO Joint Meeting on Pesticide Management (JMPM)
2. To organize a field survey in areas of agricultural activities with high use of pesticides (Morogoro, Iringa, Mwanza, Shinyanga and Arusha regions) to assess the needs and risks of current uses of HHPs, reasons for use and review of viable alternatives;
3. To conduct quantitative risk assessments for selected HHPs.
4. To elaborate a list of safer alternatives including agroecosystem-based practices and low-risk pesticides;
5. To organize a round table with key stakeholders (e.g., academia, farmer groups/associations, NGOs, pesticide industries and research institutions and identify safer alternatives and other risk mitigation measures;
6. To organize one high-level meeting to facilitate regulatory actions, contribute to pesticide regulation harmonization efforts and guidance to fast-track registration of biopesticides and other safer alternatives and
7. To develop and roll out HHP risk reduction communication/awareness products/materials
Pia Jumla ya Washiriki 187 wakiwemo wakulima Viongozi na Maafisa Ugani katika Wilaya za Same, Kilolo, Mbalali, Kigamoni, Kilosa na Karatu wamepatiwa mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya Viuatilifu ikiwa ni sehemu ya lengo la mradi.
0 comments:
Post a Comment