METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, April 24, 2022

MICHUANO YA MKENDA CUP 2022 YAHITIMISHWA JIMBO LA ROMBO KWA KISHINDO

Mabingwa wa Mashindano ya Mkenda Cup 2022, Timu ya Kata Rongai Fc wakishangilia ushindi Mara baada ya kukabidhiwa Zawadi zao(Picha zote na Innocent Natai)
Mgeni Rasmi Mhe.David Silinde Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI akikabidhi zawadi ya Fedha kwa Mshindi wa kwanza.
Mgeni Rasmi Mhe.David Silinde Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI akihutubia halaiki ya wananchi na mashabiki wa michezo waliojitokeza kushuhudia fainali za Kombe la Mkenda Cup 2022.
Mbunge wa  jimbo la Rombo Mhe. Prof Adolf Mkenda akihutubia mamia ya wananchi na mashabiki wa michezo waliojitokeza kushuhudia fainali za Kombe la Mkenda Cup 2022.
Waandaaji wa Mashindano ya Mkenda Cup 2022, wakiandaa zawadi mbalimbali kabla ya kukabidhiwa kwa washindi wa michuano hiyo.   
Baadhi ya wananchi na mashabiki wa michezo waliojitokeza kushuhudia fainali za Kombe la Mkenda Cup 2022.


Na Innocent Natai, Rombo

Michuano ya Kombe la Mbunge wa jimbo la Rombo ambaye pia ni Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof Adolf Mkenda linalojulikana kama Mkenda Cup 2022 imemalizika jana April 24, 2022 Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro  ambapo Timu Motamburu Kitendeni (Rongai Fc) ikiibuka Bingwa wa Mashindano hayo kwa Mwaka 2022.

Michuano hiyo ambayo ilikutanisha timu zaidi ya 63 kutoka katika Wilayani Rombo imemaliza kwa kuzikutanisha timu za Motamburu Kitendeni (Rongai Fc) na Ubetukae Fc, ambapo Rongai Fc iliibuka bingwa wa Kombe hilo kwa Mwaka 2022  kwa  Mikwaju ya Penati 6 kwa 5 baada ya kufungana bao 1-1 ndani ya dakika 90 na kujinyakulia kitita cha Shilingi milioni mbili pamoja na Kombe.

Huku Mshindi wa Pili Ubetukae Fc akipata zawadi ya Shilingi milioni moja, mshindi wa tatu kiasi cha Shilingi laki tano huku mfungaji bora akijipatia kiatu cha dhahabu, kipa bora akijipatia Jezi ya kipa, Gloves, na Soksi kadhalika mchezaji bora akiondoka na zawadi ya mpira.

Akizungumza wakati wa kukabidhi Zawadi mbalimbali kwa Washindi, Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. David Silinde ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika fainali ya mashindano hayo, amempongeza mdhamini wa mashindano hayo ambaye ni Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof Adolf Mkenda  kwa kusema kuwa mashindano hayo yana kwenda kuinua vipaji katika jimbo hilo na kuimarisha afya za wananchi wa jimboni hapo.

Aidha Mhe. Silinde aliongeza kuwa  Michuano hiyo inajenga uzalendo wa Vijana wa Rombo huku pia akimuomba kuiendeleza Michezo hiyo kwani imeonyesha Mafanikio Makubwa tangu kuanzishwa kwake.

“Wilaya ya Rombo ni moja ya Wilaya ambayo ilikuwa nyuma katika suala la Michezo lakini kwa Muda Mfupi sasa Wilaya hii imeonekana kuwa kinara” Mhe. David Silinde aliongeza

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Rombo ambaye pia ni Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof Adolf Mkenda ameahidi kuendelea kudhamini Michuano hiyo kwa mwaka ujao kwani kupitia michezo hiyo imefanikiwa kuwaweka pamoja vijana na wananchi wa jimbo hilo na kuwezesha hata kupangilia namna ya kuwapatia mikopo ya kujiendeleza.

“Mashindano hayo yataendelea tena mwanzoni mwa mwezi Januari 2023 lakini kwa heshima ya Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa za kimaendeleo alizozifanya Jimbo la Rombo tunaanza sasa kucheza michezo ya kirafiki ambayo itaitwa Samia friendship Tournaments “ Prof. Mkenda aliongeza 

Aidha pia amesema kuwa  michezo hiyo ya kirafiki itakayoitwa Samia friendship Tournaments itajumuisha pia michezo ya wanawake pia na wakati huo huo viwanja vya michezo wilayani hapo vikiendelea kufanyiwa maboresho






Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com