Mkurugenzi wa Asasi ya SIREWOCHA GROUP-Tanzania Enock Mwang’onda akizungumza na vyombo vya habari kwenye makao makuu ya Asasi hiyo iliyopo Manispaa ya Singida mkoani hapa.
Mkurugenzi wa Asasi ya SIREWOCHA GROUP-Tanzania Enock Mwang’onda akiwa kwenye makao makuu ya ofisi hiyo.
Mwonekano wa jengo la utawala la makao makuu ya ofisi hiyo.
Bango la anuani ya ofisi lililopo nje ya jengo la makao makuu ya ofisi hiyo.
Na
Hamis Hussein, Singida.
ASASI
isiyo ya kiserikali ya Sirewocha Group-Tanzania yenye makao yake makuu ndani ya
Manispaa ya Singida mkoani hapa tayari imeanza rasmi zoezi la kusajili makundi
ya wastaafu, wazee, walioachishwa kazi kisheria na wote wenye mahitaji maalum
maarufu ‘ombaomba’ ili kuwaunganisha pamoja na kuanza kuwapatia misaada
mbalimbali ikiwemo fedha taslimu na vifaa mbalimbali vya kujikimu kimaisha
badala ya kuendelea kuzurura hovyo mitaani
Kwa
mujibu wa Sirewocha pamoja na mambo mengine, zoezi la ugawaji wa fedha na vifaa
mbalimbali ikiwemo nguo na vyakula kwa wahitaji, simu za mkononi kwa ajili ya
kurahisisha mawasiliano, fimbo za kuwaongoza wasioona sambamba na kusajili
watoto wa mitaani ili kuwapatia misaada na kuwarejesha makwao kwa kuwaunganisha
na wazazi wote watakaokuwa na nia hiyo-kwa kila siku za Ijumaa-litaanza
Februari 4 mwaka huu.
Mkurugenzi
wa Asasi hiyo Enock Mwang’onda alisema asasi hiyo baada ya mkoa wa Singida
inatarajia kusambaza huduma hiyo kwa kuweka ofisi zake Tanzania Bara, lengo ni
kuhakikisha wanafanikiwa kuondoa ombaomba wote mitaani kwa kuanzia na mkoa wa
Singida na kuwaunganisha wote wenye mahitaji mapema ifikapo 2025.
“Tayari
tumewawekea ofisi yao hapa ambayo watakuwa wakikutana hapa kwa kila siku za
ijumaa kuanzia ijumaa ijayo (Februari 4) kupata misaada mbalimbali…lengo letu
hasa ni kurudisha hadhi na kuwajengea heshima inayostahili hawa wenzetu badala
ya kuwaacha tu wakiendelea kuombaomba mitaani,”
alisema Mwang’onda
Asasi
hiyo iliyosajiliwa Oktoba 29 mwaka jana ndani ya Manispaa ya Singida, pamoja na
mambo mengine inatarajia kusaidia pia makundi mengine ya wahitaji, ikiwemo
kuwanunulia sare za shule watoto yatima, kuanzisha miradi mbalimbali ya
ujasiriamali kwa wastaafu ili kuwapunguzia ukali wa maisha-sanjari na kuwafikia
wazee na vikongwe.
“Kwa
kuwa lengo letu ni kusaidia watu wenye mahitaji maalumu tunawaomba watanzania
wote wenye mapenzi mema na watakaoguswa na namna tunavyotoa huduma hii kutuunga
mkono kwa kuleta michango yao ya hali na mali kwenye ofisi yetu ili tuwagawie
wahitaji wa makundi haya , alisema Mwang’onda.
0 comments:
Post a Comment