METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, December 6, 2021

WATAKIWA KUONGEZA KASI YA KUPIMA ARDHI

Na Lucas Raphael 

Urambo Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Dkt Angeline Mabula ameiagiza halmashauri ya wilaya ya urambo mkoani Tabora  kuongeza kasi ya kupima na kumilikisha viwanja ili kutatua migogoro ya ardhi

Alitoa  Agizo hilo jana kwa viongozi wa wilaya ya urambo wakati wa ziara ya siku moja wilayani humo na kusisitiza kwamba lengo ni kuwawezesha wananchi katika sekta ya ardhi

Dkt Angeline Mabula Alisema umilikishaji wa maeneo yao huwa kichocheo cha shughuli za maendeleo ikiwemo kupata mikopo benki kuweka dhamana na kupunguza migororo ya ardhi

Sambamba na Agizo hilo Naibu waziri  aliipongeza halmashauri ya wilaya ya urambo kwa kufanya kazi kwa malengo yaliyolengwa na wizara licha kuwa na uhaba wa watumishi na kuwaitaka halmashauri hiyo kuitumia ofisi ya ardhi  ya mkoa ili kuwasaidia katika utendaji kazi

Awali afisa ardhi wa wilaya ya urambo Joel Mapunda alisema walikuwa wakikwamishwa na uhaba wa vitendea kazi jambo ambalo limeshatafutiwa ufumbuzi na kwa sasa.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya urambo Louis Bura aliishukuru wizara kwa kuutatua mgogoro uliokuwepo kati ya maeneo ya hifadhi na wananchi na kuongeza kuwa maagizo yake wameyapokea na wataenda kuyafanyia kazi.

Halmashauri ya wilaya ya urambo imepima na kugawa hati ya viwanja 106 kati ya viwanja 865 katika kata ya urambo .

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com